HUDUMA YA KINABII
Manabii
(Prophetes)
Neno nabii limetokana na maneno
haya “Pro ” yaani mbele, na
“ Phemi ” yaani kujulisha wazo la
Mungu au mtu, lisilojulikana.
Manabii husema mambo ya mbele
na pia ya sasa kwa uvuvio wa
Roho Mtakatifu. Kwa maana ya
pili niliyoisema hapo juu,
Mchungaji mwalimu au mwinjilisti
asemapo Neno wakati wa sasa kwa
msukumo na ufunuo wa Roho
Mtakatifu, asemapo Neno hilo la
wakati, husimama kama nabii kwa
wakati huo.
HALI HIZI IKIWA ZINADUMU
KWA MTU KATIKA HUDUMA
INAWEZEKANA NI NABII AU ANA
HUDUMA YA KINABII
(a) Nabii ni mtu awezaye kujua
wazo la Mungu la wakati na
kulisema au kulitenda.
Anaweza kuwa haitwi nabii,
lakini hali hii ni ya kinabii.
(b) Nabii anapewa neema ya kujua
wazo la moyo wa mtu na
kulisema (Matendo 5:3). Mara
nyingine wazo la Mungu
kuhusu mtu, watu au hali ya
nchi na anga la kiroho.
(c) Mungu humpa kujua ayaonayo
Yeye (Mungu) wakati ujao,
wakati wa sasa au wakati
uliopita (Matendo 11:27-30).
(d) Manabii hutengeneza misingi
iliyoharibika na kuimarisha
misingi kwa njia ya kufundisha
neno la Mungu kwa ufunuo
wa Roho. Huduma ya
mwalimu afundishaye neno la
wakati kwa ufunuo wa Roho
inaweza kuitwa mwalimu wa
kinabii.
(e) Katika Agano jipya nabii
hufanya kazi katika timu ya
huduma, sio peke yake,
hufanya na viongozi wengine
katika huduma tano. Huyu
siye mtu mmoja aliyejuu na
wengine wote wako chini yake
wakisubiri Mungu aseme
kupitia yeye tu, mfumo huu
sio wa Agano Jipya. Katika
Agano Jipya manabii hufanya
kazi katika timu (Matendo
13).
(f) Karama kuu katika huduma ya
nabii ni neno la maarifa,
unabii, neno la hekima,
kupambanua roho, mara
nyingine karama za nguvu
kama miujiza, uponyaji na
imani maalum. Kuna tofauti
kati ya huduma ya nabii na
karama ya unabii, mtu
akitumiwa katika karama ya
unabii haimfanyi yeye kuwa
nabii.
(g) Mara nyingine huduma ya
nabii hujificha katika huduma
nyingine. Kwa mfano mtu
anaweza kuwa mwalimu,
mchungaji au mwinjilisti na
hapo hapo ni nabii. Mfano wa
mtu wa namna hii ni askofu
Immanuel Lazaro.
(h) Manabii hupambanua nyakati
za kiungu na majira ya jambo
kufanyika na kuwaandaa watu
(Matendo 11:28, Matendo
21:10-11).
(i) Kila nabii ni mwombaji, lakini
si kila mwombaji ni nabii
(Yeremia 27:18). Haiwezekani
kuwa nabii bila kuwa
mwombaji, ila inawezekana
kuwa mwombaji bila kuwa
nabii.
(j) Utendaji kazi wa kinabii upo
tofauti tofauti. Kuna manabii
waalimu (Kenneth Haggin),
manabii wainjilisti(Charles
Finney), manabii wachungaji,
manabii mitume na manabii
walio manabii tu. Kuna
manabii waimbaji, pia
waombaji manabii. Wakati
wanaomba huona jambo na
kulibadilisha kwa mamlaka au
kulisimamisha kwa mamlaka.
(k) Neno la kinabii linaposemwa
ni vema lizalishwe katika
ulimwengu wa mwili kwa
maombi na maombezi, maana
adui hujaribu kuzuia kusudi
ka Mungu lililonenwa kinabii.
Mfano mtoto aliyetabiriwa
kuwa mtumishi, Neno hilo
latakiwa liatamiwe kwa
maombezi limtokee.
(l) Manabii na maneno ya kinabii
hujidhihirisha wakati maalum
( Kairos) na si wakati wote wa
masaa ishirini na nne
( Kronos). Katika Agano Jipya
huduma hii haionekani sana
pengine ni kwasababu ya
udhihirisho wa Roho
Mtakatifu na sauti ya Mungu
kwa kila mwamini.
(m)Nabii akitoa neno katika kundi
wajibu wake huisha. Wajibu
unaofuata ni wa mchungaji,
mwalimu au mtume kulithibitisha
na kulijaribu kwa maandiko na
kulihakikisha, hata kama ni Mungu
anasema (1Wathesalonike
5:20-21). Maandiko yana mamlaka
ya mwisho kuliko neno la kinabii.
Nabii lazima ajitiishe chini ya
mamlaka ya maandiko.
(n) Muhubiri, mwalimu au
mchungaji, anapofundisha Neno la
Mungu kwa uvuvio na ufunuo wa
Roho Mtakatifu na kunena Neno la
wakati, ujumbe huo ni wa kinabii.
Mgongano
Mara nyingi huduma ya nabii
hugongana na mchungaji kwa
sababu zifuatazo:
1. Nabii husema Neno, pasipo
kujali hisia za wasikilizaji.
2. Mchungaji hujali hisia za
watu zaidi.
3. Nabii hutazama ujumbe
aliopewa, Mchungaji
hutazama watu
wanaosikia, inahitajika
hekima ya kukaa na
kuvumiliana. Katika kundi
mwenye neno la mwisho
ni mchungaji, hivyo nabii
ajizoeze kujitiisha kwa
mchungaji, wakati huo
huo mchungaji
asimdharau nabii.
4. Huduma ya nabii hufanya
kazi kirahisi kwenye timu
za kitume na kiinjilisti
zaidi ya kanisani
(Matendo 13:1-3).
5. Huduma hii haionekani
sana kwakuwa hatujatii
ipasavyo agizo kuu la
kuufikia ulimwengu na
injili.
6. Baadhi ya watumishi
husema huduma hii haipo
katika Agano Jipya. Huo
sio ukweli, huduma hii
ipo ila utendaji kazi wake
ni tofauti na Agano la
Kale. Ni hatari kanisa au
huduma kuwepo bila
ufunuo wa kinabii
kuwepo wakati wote kwa
njia ya Roho Mtakatifu.
Muhimu: Mengi niliyoandika
hapa yanatokana na
ufahamu wa maandiko na
uzoefu wa sehemu katika
huduma, maishani
mwangu na watumishi
niliowahi kuwasikia au
kuwafahamu kihuduma.
