MAOMBI YA KUOMBEA UCHAGUZI WA TAIFA
Bwana asifiwe sana..leo ninahimizwa nianze kufundisha somo lisemalo..
MAOMBIYA NAMNA YA KUPATA VIONGOZI WA TAIFA KTKA KUSUDI LA MUNGU..
Kabla ya yote napenda kusema hatuwezipata viongozi kama hawakuchaguliwa na 18
Kura hukomesha mashindano; Hukata maneno ya
wakuu.
19
Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuliko mji wa
nguvu; Na mashindano ni kama mapingo ya ngome na Mungu pili na mwanadamu. lkn ktk yote huwezi kuchagua kama hakuna watu zaidi ya mmoja..Mfano Mungu ametuchagua sisi kutoka ktk watu wengi wa duniani ili tuitwe wanaye.
Kwa habari ya uchaguzi wa taifa lolote unapozungumza uchaguzi ni kama mshindano....NINAPENDA NISEME...Mambo ya Uchaguzi ni mpango wa Mungu vs usio wa Mungu..
Ninamaanisha wako wa MUNGU pia wako hawatokani na mpango wa MUNGU.MITH. 19: 18
Kura hukomesha mashindano; Hukata maneno ya
wakuu.
19
Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuliko mji wa
nguvu; Na mashindano ni kama mapingo ya ngome.
Mistari hii inaonesha kuna team mbili yaani Mpango wa Mungu vs mpango usio wa MUNGU ..Sasa wengi hatukati haya mashindano vizuri kwa kudhani Mungu hausiki hapa;wakati wa sauli tunaona watu walitaka Mungu awape mfalme wa kuwatawala lkn kumbe Mungu hakutaka afanye hivyo muda huo.sasa huo ukawa mpango wa Mungu vs mpango wa shetani..
Mungu ndiye huwaweka watawala juu ya nchi na wala si mwadamu
JINSI GANI YA KUOMBEA UCHAGUZI WA VIONGOZI?
Kwanza tambua lazima uombe kwa kanuni zifuatazo
1: Maombi ya toba ni mhimu ..
Maombi haya yatahusu taifa ;viongozi waliotangulia ;ardhi na mipaka ya nchi..
√imeandikwa... ISAYA 64:6 "Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu;na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo uliyotiwa unajisi;sisi sote twanyauka kama jani;na maovu yetu yatuondoa,kama upepo uondoavyo"
Hakika tumekaa ktk taifa lenye dhambi sisi pia tumehesabiwa na na wasiohaki tumechafuka kwa kuwa sisi ni walinzi kiroho na hatufanya wajibu wetu kama waombaji..hatukuwakemea mafisadi sasa MUNGU aturehemu ktk haya yote.
√ Tunatubu kwa kuwa kuna mikataba imefanyika kinyume na ufalme wa MUNGU... ISAYA 28:1-18
"....lisikieni neno la BWANA enyi watu wenye dharau;mnaowatawala watu haea walio ndani ya Yerusalemu.Mmesema tumefanya agano na mauti ;tumepatana na kuzimu......"
Tunahitaji kutubu kwani watawala wamekubaliana na kuzimu yaani walipokuwa wanaingia madarakani walienda kwa wachawi ili wawasaidie kumbe hapo wamejiunganisha na kuzimu bila kujua..ukiendelea kusoma inasema umefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio ...sasa unatakiwa ujue kuna watawala hujiamini lkn kujiamini kwao ni kwa sababu mganga wao anawahakikishia mambo mazuri..ni kwa kuwa kuzimu inawapa nguvu..
unaweza usinielewe lkn nikwambie wengine wanatawala kwa kafara .sasa ujue wewe umewekwa kubatirisha mambo hayo.
DAMU YA YESU NDIYO SILAHA HAPA.
KESHO NITAELEZA KIFUPI NA JINSI YA KUFANYA MAOMBI HAYA YA TOBA..
bishop eliya kasebele..
SIMAMA MAHARI PALIPO BOMOKA
KUJENGA..
Revival builders church..
PO BOX 140
RUVUMA-TANZANIA
EAST AFRICA
EMAIL..emanuelkasebelee@gmail.com
+255766891120

Maoni 0:
Chapisha Maoni
Welcome
Jisajili kwenye Chapisha Maoni [Atom]
<< Nyumbani