JINSI GANI UTAELEWA KITABU CHA UFUNUO?
Jibu: La muhimu katika kutafsiri Biblia, hasa kwa
kitabu cha Ufunuo, ni kuwa na ufafanusi thabiti.
ufafanusi ni utafiti wa kanuni za tafsiri. Kwa maneno
mengine, ni njia ya kutafsiri maandiko. Ufafanusi wa
kawaida au tafsiri ya kawaida ya maandiko ina
maana kwamba kama mstari au kifungu
kinaonyesha wazi mwandishi alikuwa anatumia
lugha ya mfano, ni lazima ieleweke katika maana
yake ya kawaida. Sisi si hatustahili kuangalia kwa
maana nyingine kama maana ya asili ya msitari una
maana. Pia, sisi hatustahili kufanya maandiko kuwa
ya kiroho kwa kushirikisha maana kwa maneno au
misemo wakati mwandishi yu wazi, chini ya uongozi
wa Roho Mtakatifu, maana ieleweke kama
ilivyoandikwa.
Mfano mmoja ni Ufunuo 20. Wengi hutoa maana
mbalimbali kwa marejeo ya Kipindi cha miaka elfu.
Hata hivyo, lugha haimaanishi kwa njia yoyote
kwamba ushahidi wa miaka elfu moja kuchukuliwa
kwa maana ya kitu kingine chochote Zaidi ya kipindi
halisi cha miaka elfu moja.
Muhtasari rahisi kwa kitabu cha Ufunuo hupatikana
katika Ufunuo 1:19. Katika sura ya kwanza, Kristo
aliyefufuka na kuinuliwa anazungumzia Yohana.
Kristo anamwambia Yohana "kwa hiyo andika, yale
uliyoyaona, na yenye yako sasa na yatayofanyika
baadaye." Mambo Yohana alikwisha yashuhudia ni
kumbukumbu katika sura ya 1. "Mambo ambayo
yalikuwa" (yaliokuwapo katika siku ya Yohana) ni
kumbukumbu katika sura ya 2-3 (barua kwa
makanisa). "Mambo yatakayofanyika" (mambo ya
baadaye) ni kumbukumbu katika sura 4-22.
Kwa ujumla, sura ya 4-18 ya Ufunuo inazungumzia
hukumu ya Mungu juu ya watu wa dunia. Hukumu
hii si kwa ajili ya kanisa (1 Wathesalonike 5:2, 9).
Kabla ya hukumu kuanza, kanisa itakuwa
imeondolewa kutoka dunia katika tukio liitwalo
kunyakuliwa (1 Wathesalonike 4:13-18, 1
Wakorintho 15:51-52). Sura ya 4-18 huelezea
wakati wa "shida ya Yakobo" -matatizo kwa ajili ya
Israeli (Yeremia 30:7; Danieli 9:12, 12:1). Pia ni
wakati Mungu atawahukumu walio kufuru kwa
sababu ya uasi wao dhidi yake.
Sura ya 19 inaeleza kurudi kwa Kristo na Kanisa,
bibi harusi wa Kristo. Akiweza mnyama na yule
nabii wa uongo na kuwatupa wao katika ziwa la
moto. Katika sura ya 20, Kristo anamfunga Shetani
na kumtupwa katika shimo la kuzimu. Basi, Kristo
anauansisha ufalme wake hapa duniani ambao
utadumu miaka 1000. Mwishoni mwa miaka 1000,
Shetani atafunguliwa na anaongoza uasi dhidi ya
Mungu. Yeye kwa haraka anashindwa na pia
kutupwa katika ziwa la moto. Kisha hukumu ya
mwisho hutokea, hukumu kwa makafiri wote, wakati
wao pia watatupwa katika ziwa la moto.
Sura ya 21 na 22 hueleza kile kinajulikana kwetu
kama hali ya milele. Katika sura hizi Mungu
anatuambia namna milele pamoja naye itakuwa.
Kitabu cha Ufunuo kinaeleweka. Mungu hangeweza
kupeana hicho kitabu kwetu kama maana yake
kamwe ilikuwa siri. Muhimu katika kuelewa kitabu
cha Ufunuo ni kukitafsiri kijuu juu iwezekanavyo-
kinasema chenye kinamaanisha na kumaanisha
chenye kinasema.

Maoni 0:
Chapisha Maoni
Welcome
Jisajili kwenye Chapisha Maoni [Atom]
<< Nyumbani