MITUME
Katika Agano Jipya tunaona mitume wakitajwa kama mara 80 hivi, kwahiyo kwa vyo vyote katika kanisa la kwanza walikuwa ni watu muhimu, na kwa kweli ~ Mitume ni ‘wa kwanza’ kanisani (1Kor 12:28). Kanisa limejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii (Efe 2:20). Mitume na manabii wana ufunuo maalum na uwezo wa kuelewa mambo kutoka kwa Mungu (Efe 3:5) (Yud 1:17). Makanisa yanapaswa kuwa na mitume wao (2Pet 3:2).
Lakini je, mitume ni kwa ajili ya siku zetu pia au walikuwepo mwanzo kwa kazi ya kuanzisha Ukristo?
Kama hata sasa wanatakiwa, ni akina nani hao na wanafanya nini? Sisi Tunafanya Nini?
Leo hii tunaongozwa mara kwa mara na watawala au wachungaji wenye karama, lakini kama mitume bado ni ‘wa kwanza’ wa Mungu katika kanisa na moja ya misingi yake, tunapaswa kufanya nini?
Mtume Ni Nani?
Neno Mtume lina maana ya mtu anayetumwa, na kupewa uweza wa kufanya umisheni kutoka kwa Mungu. Utume si cheo, ni wito, ni karama na shughuli kama shughuli nyingine yo yote ndani ya kanisa. Mitume Katika Agano Jipya Yesu, yu juu ya wote, (Ebr 3:1). Wale mitume thenashara wa Mwanakondoo (Mk 3:14-16) (Mdo 1:26) (Ufu 21:14). Karama ya mtume (Efe 4:11); watu kama Paulo, Yakobo, Barnaba, Timotheo, Sila, Andronika na Yunia. Biblia haijatuambia kwamba hawa walikuwepo kwa ajili ya karne ya kwanza peke yake. Kutokana na ukweli kwamba Kristo aliweka wengine kanisani kuwa mitume ili kutenda kazi ambayo bado haijakamilika (Efe 4:12-14) ni ushahidi tosha kwamba mitume wanahitajika sana hata leo kama karama nyingine zilizozoeleka zaidi (Efe 4:11).
Ni Nini Kazi Za Mtume?
Si kila mtume anayetenda kila kazi kama inavyoonekana katika Agano Jipya lakini kazi za kitume ni pamoja na ~
Kueneza injili, kwa mfano safari nyingi za Paulo, na ziara ya Petro kwenye eneo lile ambalo halikuwahi kufikiwa kabla katika nyumba ya Mmataifa (Mdo 10). Kuwafikia watu ambao hawajafikiwa (Rum 15:20). Kusababisha uinjilisti mpya kufanyika (Mdo 19:10). Kusababisha makanisa mengi mapya kuanzishwa, kama alivyofanya Paulo kusini mwa bara la Ulaya. Kuwa mjenzi mkuu mwenye hekima, anayejua la kufanya (1Kor 3:10; 5:3; 6:4; 7:1; 8:1). ®Mitume Huweka Misingi Imara Ya Kristo (1Kor 3:11) Ya maisha katika Roho (Mdo 19:1; 8:14-17). Ya utii mbele za Mungu (Rum 1:5). Ya fundisho la kweli (Efe 3:2-21) Ya viongozi wazuri (Mdo 14:23) (Tit 1:5).
® Kuwa baba au mama wa makanisa machanga, kuyatia moyo kwa nyaraka na ziara, na kamwe si kuyadhibiti (2Kor 11:28) (1The 2:7,11).
® Kukabiliana na tamaduni zisizo na maana, kama Paulo alivyopingana nazo hata kwa Petro (Gal 2:11-14). Safari za kuuunganisha Mwili kama alivyofanya Paulo akiunganisha Yerusalemu, Antiokia na makanisa mapya kwa mahusiano yake. Alionesha urafiki wa muda mrefu na uaminifu, akitenda kazi katika mahusiano na si katika mifumo na vyeo (1The 1: 5-7; 2:8) (Flp 1:8; 4:10,14,15) (Mdo 20:31; 18:11).
•Utamtambuaje Mtume?
Mitume huitwa na Mungu, na wakajua, na watu wote pia. Wanaweza wakakubali wito wao, lakini hawana haja ya kutangaza nafasi yao kama cheo, na haipaswi kuwa hivyo, badala yake ni nafasi yenye majukumu makubwa. Angalia salamu za Paulo anavyoanza kuandika nyingi ya nyaraka zake; na pia angalia uone kwamba mitume ~ Wanatambuliwa na viongozi wengine wa kanisa (Mdo 15:2,4). Wanatenda kazi na kuonesha ushuhuda wa wito wao si kwa kulazimisha na kudhibiti wengine, bali kwa kuendelea kuweko udhihirisho wa uweza wa Roho (2Kor 11:6-13). Wanao watu kama uthibitisho hai wa huduma yao (2Kor 3:2,3). Wamepakwa mafuta kwa ajili ya huduma (2Kor 12:12). Wamemwona Mungu wao wenyewe katika historia ya ustahimilivu katika shida na upinzani (2Kor 12:7-10) (1Kor 4:9-13). Mitume Pia
•Wanahitaji Makwao
Mitume katika Agano Jipya wanaonekana sikuzote wakitenda kazi katika timu ya umisheni au pamoja na wazee wa kanisa nyumbani ambako ni kituo cha kitume Angalia Matendo 15 na somo la 12.
•Ni Nini Kituo Cha Kitume?
Ni kanisa la mfano, ambako mitume, timu mbalimbali na watu wanakusanyika pamoja kwa ajili ya Yesu na kwa ajili yao wenyewe kwa wenyewe. Ni mahali pa kuanzia na kituo cha kupatia watu, fedha na vifaa kwa ajili ya umisheni. Ni mahali pa ushirika, pa kuhuishwa, pa kuwajibika na kuwategemeza wale wanaofanya huduma za kitume, na kamwe isiwe piramidi ya huduma yenye ‘mtume aliyewazidi wenzake’ akiwa kwenye nafasi ya juu akitoa amri tu. Ni pale tu timu ya Paulo ilipokuwa nje ya kituo huko Antiokia ndipo walipojitawala na kujitegemea (Mdo 14:26-28).
•Vituo Vya Kitume Katika Biblia•
Makanisa ya Yerusalemu, Antiokia, Efeso na Thesalonike yalikuwa ni zaidi ya makanisa ya maeneo tu. Haya yalikuwa na huduma katika Roho Mtakatifu yakifanya maombi, uinjilisti, unabii, mikutano ya mafundisho na ibada. Kulikuwa na viongozi kadhaa, kanisa lililo hai na ushirika. Walikabiliana na changamoto za kisheria, mateso, mkakati na kupeleka timu za kitume na kuusaidia ulimwengu wa Wayahudi, na kuendelea hadi Samaria na hatimaye kwa mataifa.
•Ni muhimu kwamba mitume wajifunze nyumbani na kisha wawapelekee wengine hayo masomo. Ni lazima vituo vya kitume vifaulu mtihani wo wote, na pawe ni mahali ambapo timu za kitume zinaona fahari kuelekeza watu na kuwakaribisha kuja kujifunza.

Maoni 0:
Chapisha Maoni
Welcome
Jisajili kwenye Chapisha Maoni [Atom]
<< Nyumbani