Ijumaa, 5 Desemba 2014

MAOMBI NINAKUOMBEA KUHARIBU MIKONO YA KICHAWI

Mikono ya wachawi waliowahi kugusa mikono yangu nguo zangu, chakula change, mali zangu zote kuanzia sasa kwenye ulimwengu war oho ninafuta alama zao kwa jina la Yesu.
Kila unapoamka unapoomba unatakiwa uombe kwa damu ya Yesu ninaitakasa mikono yangu uso wangu, mwili wangu ninaitakasa kwa damu ya Yesu. Usiwaogope na kwa kwa kuwepa unatakiwa upambane nao kwa jina la Yesu. Kila aliyegusa nguo yako kwenye ulimwengu wa roho leo tunamrudishia vyote alivyoviweka kwa jina la Yesu.Ukiguswa na Mungu ile nguvu inaingia mpaka kwenye mifupa ndani ya mwili.
Kwa jina la Yesu mikono ya kichawi iliyogusa vitu vyangu mwili wangu au kitu chochote ninavifuta kwa jina la Yesu, alama za kichawi zilizoachwa ndani ya nguo zangu ninazifuta kwa damu ya Yesu, mikono ya kichawi iliyogusa ndoa yangu, familia yangu, kazi yangu ninaamuru kwa jina la Yesu ivunjike kwa jina la Yesu kristo, ninanyoosha mkono wa Mungu kuivunja na kuiteketeza mikono ya kishetani iliyo nyooka juu ya maisha yangu ninaivunja kwa jina la Yesu kristo,imeandikwaUFUNUO12:11 “nao wakamshinda kwa damu ya mwana kondoo” kila mchawi aliye nyoosha mkono wake juu ya mwili wangu, nguo zangu, kichwa changu, kanisa langu, nchi yangu, ndoa yangu, nchi yangu ninaipoozesha kwa damu ya mwana kondoo, kwa jina la Yesu kristo.
Kila mkono wa kishetani ulionyooka ili kuleta maangamizo juu yangu ninaupoozesha na kuuvunja kwa jina la Yesu kristo, ninatuma polio kwenye mikono yote ya kichawi iliyojipanga kugusa watoto wangu, biashara yangu, elimu yangu ninaipoozesha kwa damu ya Yesu kristo, ninaivunja kwa jina la Yesu kristo. Kila kazi iliyoanzishwa na mikono ya kishetani ninazibatilisha kwa jina la Yesu kristo, ninaamuru kwa mamlaka ya Jina la Yesu kila mkono wa kichawi ulionyooka kunigusa mimi na familia yangu ninaipoozesha kwa damu ya Yesu krito ninaipoozesha kwajina la Yesu, ninaifyeka kwa jina la Yesu kristo.
Mikono inayoleta utasa ninaivunja kwa jina la Yesu ewe mkono ulionyooka kuleta utasa kazini kwangu, utasa kwenye elimu ninakuvunja kwa jina la Yesu kristo, kila mkono wa kichawi uliotumwa kunigusa mimi na vyote nilivyonavyo leo ninakuvunja kwa jina la Yesu kristo, ewe shetani uliyenyoosha mkono wako kuniletea uoga wakati wa usiku na hofu wakati wa mchana leo ninakuvunja kwa jina la Yesu kristo, kila mkono ulionyooka kwa watoto wangu, wazazi wangu, rafiki zangu, na ndugu zangu wote leo ninaondoa uweza wako wa kudhuru na kukuvika polio upooze na ninakufyeka kwa jina la Yesu kristo, ninaukata mkono ulio nyooshwa ili nisiolewe kwa jina la Yesu, ninaukata mkono ulionyooshwa ukagusa nguo zangu, mali yangu au chochote nilicho nacho kwa jina la Yesu, ninaukata mkono ulionyooshwa kugusa ajira yangu kwa jina la Yesu, ninaukata mkono wa wachawi ulionyooshwa kugusa mapato yangu kwa jina ya Yesu, mchawi mwanaume,mtoto,mwanamke, mzee ninaukata mkono wako uliounyoosha kunigusa mimi na mali zangu kwa jina la Yesu kristo.Amina.

Maoni 0:

Chapisha Maoni

Welcome

Jisajili kwenye Chapisha Maoni [Atom]

<< Nyumbani