Jumatano, 1 Februari 2017

USIJIANGAMIZE MWENYEWE

Haleluya wana MUNGU ninayofuraha kubwa kukuletea ujumbe huu siku ya leo.

Yakobo. 3:2-14.
Mara nyingi watu tunahitaji sana kufanikiwa na kufika mahali tunapotoka lkn ipo shida ambayo ipo kwetu inasumbua na kutufanya tushindwe kufika tutakako. Shida kubwa inayotufelisha na ukiri wetu ktk kinywa(Ulimi)
Ni rahisi kujua unatakiwa ujue ulimi nini na unasehemu gani ktk mambo uliyokusudia kwenye maisha:-)
ULIMI NI SAWA NA USUKANI.
Usukani unaelekeza chombo kikubwa ktk mwelekeo anaotaka dreva,sasa wewe ndie dreva ila ulimi ni usukani wa mwili wako,maisha yako.
Sikia ni kwamba unatakia ufahamu kuwa unachotaka au unakotaka kufika lazima ulimi/usemi wako unene kama matakwa au nia yako ilivyo,huwezi fika unataka kwenda wakati kinywa au usemi wako unanena tofauti, ok ni jambo rahisi tu, Yesu anatuambia kuwa kila mtakalolifunga duniani limefungwa mbinguni, sasa hatufungi kimya,tunafunga kwa kunena,unahitaji usema il i yatokee, jambo lolote ktk ulimwengu wa roho haliji ktk ulimwengu wa mwili mpaka umelisemea ulimwengu huu ukatii na kuruhusu, ok kumbe kinywa chako kinauleta ulimwengu wa roho ktk ulimwengu wa mwili,ni rahisi tu kuelewa biblia inasema ulimi ndio huleta laana au baraka mst wa 10*
KUMBE...,mwelekeza laana au baraka ni ulimi/kinywa chako.
Kifo/mauti ya mafanikio yako,ndoa yako,na familia yako ipo ulimini mwako.
Mith 18:20-21a
."Mauti na uzima huwa ktk uwezo ktk uwezo wa ulimi."
Kumbe uwezo wa kufanikiwa au kushindwa ni vile wewe unaweza kutamka juu ya jambo fulani, mst wa 20*unasema tumbo hujazwa matunda ya kinywa, matokeo ya kusema kwako ndio mfumo utakaoishi .
ULIMI NI MOTO.yakobo 3:6
Ulimi ndio chanzo cha uharibifu mkubwa, tafakari moto unaweza kuwa mdogo ukasababisha msitu mkubwa ukawaka na kuteketea, msitu wa mambo yako makubwa,unaweza ukauangamiza kwa sekunde tu, hili litatokea ukiamua kuyasemea vibaya, maono yako yanaweza kufa kwa kuamua kuyatamkia vibaya,watendakazi kwenye huduma yako wanaweza kuharibika kwa kuwatamkia uharibifu. Makanisa mengi yanashindwa kufanikiwa shida ni kuwasemea wanaowaongoza laana.
Mungu aliponifundisha nilibidi nibadili jinsi ya kuongea na walionyuma yangu kwani ningezuia mfumo wa mafanikio ya huduma yangu, usikubali kuwasha moto mbaya kwa ulimi wako, jifunze kutumia maneno yako vizuri,tumia ulimi wako kujishibisha mema,.
UBALIKIWE

Lebo:

Maoni 0:

Chapisha Maoni

Welcome

Jisajili kwenye Chapisha Maoni [Atom]

<< Nyumbani