MAOMBI YA KUMILIKI
SEHEMU YA TATU.
Aina za falme 2 katika ulimwengu wa roho
(kutoka sehem ya 2).
1: UFALME WA MUNGU(NURU )
2: UFALME WA SHETANI(GIZA).
Kama nilivyotangulia kusema katika sahemu ya pili
kwamba zko falme mbili katika ulimwengu wa
roho.Na ili falme hizi zote mbili ziweze kuwa na full
control (umiliki)wa Eneo husika ni lazima
wafanikiwe kumiliki Anga,Ardhi na watu.
Note vitu hivi:-
a)–ufalme usio na watu sio ufalme,
b)–ufalme usio na mipaka yake sio ufalme,
c)– ufalme usiokuwa na umiliki wa anga sio
ufalme.
Kwa hiyo ili falme moja kati ya hizi ziweze
kuthibitika ni lazima zimiliki Anga,Ardhi na watu
eneo husika.Hii inamaanisha kuwa ili shetani aweze
kuwa na full control ya Eneo husika ni lazima amiliki
anga ,Ardhi na watu.Anapofanikiwa kufanya hivyo;
ufalme wake unathibitika,na yeye ndio anakuwa
mfalme wa eneo hilo.
Sehemu ya anga ndiko shetani anapowaweka wakuu
wake wa utawala wake yaani wakuu wa giza-
mf.belizebuli .(Biblia ya kiingereza inasema "Evil
spirits who overrules the kingdom…..)roho
zitawalazo. marko.3:27,mat.12:29 .Yesu
anawatambulisha kama “mtu mwenye
nguvu”.Ukitaka kufahamu ni jinsi gani hao wakuu
walivyo fananisha na jinsi lilivyo jeshi letu(ranking)
;huwa kuna amiri jeshi mkuu(rais),mkuu wa
majeshi,majenerali,luten,kapten nk.Kwa sababu
mimi si mwanajeshi,nadhani ni vyema ukimpata
mwanajeshi yeyote yeye anaweza kukuelezea zaidi
mtiririko mzuri wa hierarchy ya jeshi.
Hii inamaanisha kuwa katika kila mji
nchi,familia,kanisa nk.shetani ameweka wakuu
wake(mf.jinsi rais wa nchi anavyoweka wakuu wa
mkoa katika kila mkoa)- kumbuka kuwa
nimekuambia kuwa wakuu hao (wa anga) ni ile
roho au zile roho zinazotawala eneo
husika,sanasana ile iliyoanza kuwepo kwenye eneo
hilo.
-Kwa hiyo ufalme wowote kati ya hizi mbili
unapofanikiwa kuteka eneo lolote basi jua kuwa
Anga,Ardhi na Watu wote watamilkiwa na ufalme
huo.
Daniel.10:12-13,20. Kufanikiwa kwa Daniel na wale
wenzake ni kutokana na maombi yao juu ya mji na
nchi waliyokuwa wanaishi(Babeli).Daniel alipata
kibali mbele ya mfalme wa babeli,lakini viongozi
wengine wa taifa lile hawakufurahia na ndio maana
walitunga hila ya kumuua ili wao wapate nafasi ile
[ Daniel.6 ].
Esta.3- Hamani alitaka kuwau wayahudi wote
kwasababu tu alichukia kumwona mordekai na esta
katika uongozi, kilichowaokoa wayahudi ni maombi
yao.Wayahudi walichukiwa kwasababu sheria zao
zilikuwa zinapingana na sheria za miungu ya akina
hamani.
Katika nyakati za leo,kama tutashindwa kuombea
miji,nchi na maeneo tunayoishi, itakuwa ni vigumu
sana kupata viongozi wazuri.Kwasababu asilimia
kubwa ya maeneo tunayoishi yako chini ya utawala
wa giza.Na utawala wa giza wakiwemo wachawi
hawako tayari kuona miji au maeneo yao
yanamilikiwa na viongozi kutoka kambi ya Adui
(ukristo(waliookoka).Maana wanajua kuwa kiongozi
akiwa ni wa kutoka kambi ya upinzani(ukristo) basi
utawala wao uta pata shida. NB: Tatizo kubwa
walilonalo wanamaombi wengi katika kuomba kwa
ajili ya Mungu kutupa viongozi wazuri , ni kwamba
wanasubiria mpaka vyama vya siasa
vimewachagulia viongozi, ndio wao wanaanza
kumwomba Mungu awape kiongozi mzuri kati ya
wale waliochaguliwa na chama.Kumbuka kuwa
chama hakina Mungu na wazee wengi wa vyama
hawana Mungu na ndio wao wanaopanga mwaka
ujao raisi awe nani hata kama ni mbaya wanachojali
wao ni masilahi yao na ya chama nasio ya
nchi.Kama tunataka kiongozi mzuri katika nchi yetu
ya Tanzania au katika miji tunayoishi, ni lazima
tuanze kuwaombea kuanzia leo kabla ya mwaka
2015.
Utatambuaje jina la mkuu wa giza(anga-mtu mwenye
nguvu) anayemiliki eneo unaloishi?
· Angalia ni matendo gani ya giza yametawala eneo
hilo.
Kwa mfano:utakuta katika mji Fulani uchawi ndio umeenea
sana na hata habari zinazozungumziwa ni uchawi
na uganga;wakati mwingine utakuta mji unasifika
kwa vitendo vya mauaji,uzinzi/uasherati,ajali
mafarakano na ulevi na vifo vya kiroho .Kwa namna
nyingine unaweza ukatambua jina la mkuu wa giza
(anga) wa eneo unaloishi kwa kuangalia ule uovu
ulioanza kabla ya maovu mengine , kumbuka kuwa
kila uovu unaotendeka kuna pepo nyuma
yake;uzinzi unasababishwa na pepo la
uzinzi.
-
Mara nyngi unapokuta sehemu kuna mafarakano
ujue umesababishwa na mapepo kama ya
kiburi,majivuno,uchawi na uhasi.
v [Daniel.10:12-13;20].
Kitabu hiki cha danieli kinatuonyesha kuwa
aliyekuwa anamiliki anga la uajemi na uyunani ni
ufalme wa giza.Na ndio maana wakina Daniel na
wenzake walikuwa wakipigwa vita kwa sababu
walikuwa wanaenda kinyume na ufalme uliokuwa
unatawala anga la uajemi-babeli(yaani ufalme wa
giza).Na ndio maana wakina meshack,shedrack na
abedinego walitupwa kwenye tanuru la moto na
Daniel akatupwa kwenye tundu la simba.
Na kwa kwaida siku zote shetani anawatumia
wanadamu wenzetu katika kukamilisha kazi zake
hapa duniani-mf.kule Babeli-aliwatumia viongozi.Na
ndio maana mtume Paulo anatuambia kuwa
tuombee wale wanaotutawala(viongozi).
Kwa hiyo ili ufanikiwe na kazi ya Mungu ifanikiwe
ni lazima ujifunze kuombea mji unaoishi;kinyume na
hapo ni kutokufanikiwa na kupigwa vita kila
siku.Kwa hiyo usipomiliki anga na ardhi,kwa kweli
utakosa Breakthrough(mpenyo) katika maombi yako
na hata kwenye mafaniko
kimaisha,kimasomo,kibiashara na kwenye huduma
yako[kiroho na kimwili].Pia fahamu kuwa mfalme
humiliki kwa maneno yake –yeye huwa anaagiza tu
kwamba ifanyike alafu inafanyika.Pia wafalme
kipindi cha agano la kale walikwenda vitani;kwa
hiyo nawewe unatakiwa uingie vitani inapobidi.
[ 1Nyak.20:1, 2Nyak.20:20-23]
Nb: Kufanikiwa kwa Mji unaoishi ndipo na wewe
utakapofanikiwa kwa hiyo usiache kuuombea,na
kuutakia amani mji huo unaoishi.
Yeremia.29:5-7 inasema hivi “Jengeni nyumba
mkakae humo….kautakieni amani mji
ule….mkauombee Kwa Bwana, Kwa maana katika
amani ya mji huo ninyi mtapata amani”
Wewe kama mfalme wa eneo unaloishi ni
lazima uhakikishe kunakuwa na usalama juu ya
watu wako(raia) aliokupa Bwana ,pia uhakikishe
kuna ulinzi wa kutosha kwenye anga,ardhini na
majini(toba ya damu ya Yesu kila siku juu ya
maeneo hayo).Kumbuka kuwa mwanzo nilikuambia
kuwa huduma hii ya ufalme haiendi au haijitegemei
peke yake bali inategemea huduma ya ukuhani
yenye upatanisho ndani yake na katika kuhakikisha
ulinzi wa maeneo hayo manne yaani
ardhi,anga,watu na maji na maeneo unayoishi, ni
lazima huduma ya ukuhani iingie kazini.
KAZI YA UKUHANI :
· Kufanya maombi ya toba kwa ajili ya
ardhi,anga,maji(bahari,mito na maziwa) pamoja na
watu,kuta na malango ili kutakasa.[ Neh.12:30 ]
· Kufanya maombi ya upatanisho-ili kurejesha
mahusiano ya mwanzo yaliyopotea baina ya Mungu
na watu wake na eneo husika.[ kut.32:32 ]
· Kutengeneza mahali palipobomoka na kuzuia hasira
ya Bwana kwa njia ya Toba ya Damu ya Yesu.
[Eze.22:30-31 ]
-Kusimama mahali palipomoka maana yake ni
kusimama katikati ya.Maana yake unasimama
katikati ya Mungu na ndugu zako au mtu mwingine
ambaye unataka kumwombea toba au maombi
yoyote na pia kusimama katikati ya Mungu na mji
au nchi yako,mfano mzuri ni ibrahim
[ Mwanzo.18,19 ].Kwa hiyo Mungu amekuinua wewe
kama mwombezi kwa ajili ya mji,kanisa,familia na
nchi uliyoko na hata biashara za eneo hilo.
· Wewe kama kuhani unapoombea mji au nchi
(ardhi,anga,na watu) ni lazima ujue jinsi ya
kuwaombea watu hao na mji huo,yaani omba kama
mama au mzazi anayemwombea mtoto wake(omba
kama unajiombea mwenyewe).Na mfano mzuri ni
maombi ya Musa naya Daniel[ Daniel.9:4-19 ].
Maana Mungu anamtafuta mtu wa kufanya maombi
ya kikuhani kama ya Daniel.[ Eze.22:30-31 ],au ya
Musa[ Kut. 32:32].
Pia fahamu kuwa unapookoka unakuwa mfalme na
kuhani maana yake ndugu zako wote wako chini
yako na pia mji na watu walioko ndani yake wote
wapo chini yako.Wewe ndio mwenye final say &
final decision(maamuzi ya mwisho).Maana yake
ukisema “No” inakuwa “No” ukisema “Yes” inakuwa
“Yes” ndio maana Mungu akakupa funguo za ufalme
wa mbinguni [ Mathayo 16:18-19].
Wewe kama kuhani,unayo nafasi mbele za bwana
ya kumwomba Mungu kwamba Mungu awaokoe
ndugu zako,yaani wasife katika dhambi na Mungu
akafanya hivyo.Mfano,Ibrahim alimwomba Mungu
amwokoe ndugu yake Lutu asipatwe na ile adhabu
yamoto juu ya sodoma na gomora.[ Mwanzo.18,19 ]
.Pia Musa aliomba Mungu asiwaangamize waisrael
na Mungu akamsikia.pia Mungu anakuheshimu sana
unapokuwa kuhani na mlinzi. [Eze.3:17-21 ].
Watu wengi wamekuwa wakifa kwa magonjwa,na
wengine kwa ajali na huwa wengi wanakufa wakiwa
na dhambi na direct wanakwenda motoni.Hii ni
kwasababu makuhani na walinzi(wanamaombi)
wameshindwa kusimama katika nafasi zao.
UTAJUAJE KUWA ANGA LINAMILKIWA NA ADUI?
I: Upinzani mkubwa katika kumtumikia Mungu.
Utakuta kila unapojaribu kumtumikia
Mungu;ndugu,jamii,bosi kazini, wote wanakupiga
vita. Marko.5:1; -katika sura hii unaweza ukadhani
kuwa ni wale watu ndio walioamua kumfukuza
Yesu katika mji wao,la hasha hapana.Bali ni
kwamba mji ule na anga lake na watu wake
walikuwa wanatawaliwa na kumilikiwa na adui na
ndio maana badala ya kufurahia muujiza ule na
kumkaribisha Yesu kwa ajili ya muujiza alioufanya
kwa yule mtu aliyekuwa ameshindikana kwa muda
mrefu wao wakaamua kumfukuza kwenye kijiji
chao.
Matendo.4:1-5,18.
II: Ugumu wa kuomba (mpenyo wa maombi unakuwa
mdogo )
Mara nyingi utajikuta unashindwa kuomba;
unapofika muda wa maombi unaanza kupatwa na
usingizi mzito na muda mwingine unakuwa unapiga
miayo tu.
III:Vifo vingi vya kiroho na vya kimwili.
Watu wengi wanaokoka lakini baada ya muda
mchache wote wanarudi nyuma.
IV: Kupoa kiroho kwa watumishi na wanamaombi wengi.
-Utakuta watu walikuwa na kasi na juhudi katika
wokovu lakini baada ya muda wanakuwa
vuguvugu.ufunuo.3:14-21
V: Kuenea kwa mafarakano kwenye kanisa,
familia,miji,nchi n.k
-Makanisa mengi leo hii yamejawa na migogoro;
wachungaji dhidi ya wazee wa kanisa
wanagombana n.k
VI: kushamiri kwa matendo ya giza(maovu)
-Kama anga linamilikiwa na adui si ajabu kukuta
uzinzi, uasherati, ujambazi, uchawi na kila tendo
chafu na ovu la giza.Yote hiyo ni kwasababu tayari
mji huo umekuwa makazi ya mapepo.
Ufunuo.18:2 “…umeanguka,umeanguka Babeli
ule mkuu;umekuwa maskani ya mashetani,na
ngome ya kila roho mchafu,na kila ndege mchafu
mwenye kuchukiza”
-Hizi ni baadhi ya alama chache tu za kujua kama
Anga linatawaliwa na Adui au la!
KWA NINI UMILIKI MJI(ARDHI,WATU NA ANGA
LAKE?
I: Lazima umiliki mji,anga n.k, kwa sababu wewe ni
mfalme tena ni kuhani wa Bwana. Na kama wewe ni
mfalme na kuhani wa Bwana kama biblia isemavyo
katika kitabu cha; Ufunuo.5:9-10, Basi ujue kuna
eneo ambalo wewe unatakiwa ulitawale kama
mfalme wa eneo hilo.
Na ili ufalme wako uweze kuwa na nguvu ni lazima
umiliki Anga,Ardhi,na Watu.Kinyume na hapo ufalme
wako hauwezi kuthibitika na ufalme huo uko
mashakani-wewe unafikiri ni kwasababu gani
Tanzania tuna jeshi la Anga,nchi kavu,majini n.k-
Jibu ni kwasababu ya kulinda Anga,ardhi,maji na
raia wa Tanzania-na ndio maana ni lazima ujizoeze
kuombea Anga,Ardhi,maji na watu wa sehemu
unakoishi.
Usipoombea mji na Anga unakoishi basi jua kuwa
utakuwa kila siku unapigwa vita na kukutana na
vikwazo kwenye kumtumikia kwako Mungu, kwenye
uchumi, afya yako,na biashara yako n.k.Yesu
alisema kesheni muombe msije mkaingia majaribuni
[Mathayo.26:41].
Hivyo kama unataka breakthrough (mpenyo) kwenye
maisha yako ya kiroho na ya kimwili ni lazima
umiliki mji,watu na anga la eneo
unaloishi;ukishindwa kufanya hivyo basi jua utapata
vita kubwa sana,kiroho na kimwili.
II:Kwasababu kufanikiwa kwa mji unaoishi ndipo na
wewe utakapofanikiwa kiroho na
kimwili.Yeremia.29:5-7.
-unapoombea mji unaoishi utasababisha kuuepushia
mji huo na maangamizi na majanga kama vile
ajali,vita,mafuriko,moto,tsunami n.k
· E zekiel.22:30 , Bwana anamtafuta mtu atakaye
simama ili kuuombea mji ili hasira ya bwana
isimwagwe kwenye mji.ukisoma vizuri sura hii ya
ezekiel.22 utaona kuwa kinachosababisha Bwana
atake kumwaga hasira yake ni kwa sababu ya
maovu kama uzinzi, rushwa n.k
· Isaya.62:6-7, Bwana anasema kuwa ameweka
walinzi juu ya mji wa yerusalemu.Pia katika mji
unaoishi Bwana ameweka walinzi na mmoja wapo
akiwa ni wewe .Na unapokubali kuwa mlinzi ni
lazima uwe unaomba maombi haya “ufalme wako
na uje na mapenzi yako yatimizwe…”.Ufalme wake
uje wapi?ni kwenye mji unaoishi.
-Hii inamaanisha kuwa unapoomba maombi haya
ufalme wa Mungu unakuja na kumiliki na kutawala
mji, anga lake, na watu waishio ndani yake.
Lakini kabla ufalme wa Mungu haujaja ni lazima
utumie hiyo nafasi ya ukuhani uliyopewa kwa ajili ya
kutengeneza na kutaarisha mazingira ya ujio wa
ufalme wa Mungu kwenye mji unaoishi.Yaani
uachilie maombi ya toba ya Damu ya Yesu kwenye
mji,ardhi yake,anga lake na watu wake.
- Nehemia .12:30 , inasema hivi; “Na makuhani na
walawi wakajitakasa, wakawatakasa watu, malango
na kuta”
Toba yako ya mara kwa mara + Maombi ya kuombea
ufalme wa Mungu uje kwenye eneo
unaloishi .Yatakufanya umiliki mji na anga la eneo
unaloishi.
III: Kwasababu sisi ni uzao wa ibrahimu.
-Bwana alimwambia ibrahimu kuwa wazao wako
watamilki malango ya Adui zao na miji ya adui
zao. Mwanzo.22:
SEHEMU YA NNE(4):KANUNI…
JINSI YA KUTEKA NA KUANZA KUMILIKI MJI NA ANGA
AMBALO ADUI AMESHALISHIKILIA TAYARI.
· Kwanza fahamu jambo hili kuwa aliyeumba Dunia,
mbingu (anga) na vyote vijazavyo ni Mungu .Hii
inamaanisha kwamba hata mji unaokaa ni Mungu
ndiye aliyeuumba, hata sehemu anakoishi shetani ni
Mungu (YESU) ndiye aliyeumba vyote
hivyo. Yoh.1:1-5 . “…..vyote vilifanyika kwa
huyo,wala pasipo yeye hakikufanyika chochote
kilichofanyika….”
-Kwa hiyo shetani hakuumba chochote bali yeye
aliumbwa tu.Zaidi sana alichokiumba yeye ni
dhambi na maovu tu.Hivyo unapoona anamiliki eneo
fulani jua kuwa; kuna uhalali au kibali fulani
amekipata kutokana na dhambi na maovu
yaliyotendwa na yanayotendwa na watu katika mji
husika(huo).
-Shetani ni mvamizi ni sawasawa na jinsi wakoloni
walivyofanya kwa waafrika, kwa kuwavamia na
kuwatawala.Kwahiyo unapoona shetani analimiliki
eneo fulani jua kuwa ana haki/uhalali fulani
ameupata kutokana na maovu na madhambi
yanayotendeka katika mji huo.Pengine ni mazindiko
yaliyofanywa na mababu,uzinzi,uchawi
unaotendeka kila siku n.k.
· Mathayo.4:8.
-Wewe unafikiri ujasiri huo shetani aliutoa wapi wa
kuthubutu kumwambia muumbaji wake(Yesu)
[ Yohana 1:1-5 ]kuwa akimsujudia yeye atampa mali
zote za ulimwengu huu.
-Shetani alipata uhalali wa kumiliki Dunia hii baada ya
dhambi ya akina Adamu na hawa.
-Ili sasa uweze kulimilikiAnga sharti au kwanza
ufanye toba ya Damu ya Yesu kwa ajili ya Eneo
hilo .unapo achilia maombi ya toba ya Damu ya
Yesu, kwenye Eneo lako kinachotokea ni kwamba
ule uhalali wa shetani wa kumiliki hilo Eneo
unaondolewa au unafutwa na damu ya Yesu
.Halleluya!.
Baada ya kufanya maombi ya Toba ili kuliteka Eneo
hilo ni lazima ujue jinsi ya kufunga wakuu wa giza
(Anga) na kuwaseta kuzimu
Marko.3:27, Mathayo 12:29.
Kabla sijaendelea labda nikukumbushe kuwa hawa
wakuu wa giza mara nyingi hukaa kwenye maeneo
matatu hapa duniani.
i).Kwenye Anga-roho hizi chafu zinazotawala Eneo
kubwa mfano; nchi, miji n.k hukaa kwenye Anga.
Mfano: Daniel 10:12-13,20.
-Mkuu wa ufalme wa uajemi
ii).Roho chafu zitawalazo ndani ya kanisa familia n.k
-Hawa hukaa ndani ya mtu kutokana na uhalali
walioupata kutoka kwa wazazi,mababu,na dhambi
alizozitenda mtu huyo au hukaa katika anga pia.
iii).Ardhini.
- uhalali wa kukaa kwenye ardhi wanaupata
kutokana na
matambiko,mazindiko na makafara yanayotolewa kila
siku.
Mfano: marko.5 yule mtu aliyemilikiwa na jeshi la
mapepo.
UFANYE NINI ILI UFANIKISHE UTEKAJI WA MJI HUO .
Sasa basi ili uweze kuteka mji,anga n.k na kuumiliki
ni lazima kwanza uwe umeshafanya toba ya Damu
ya Yesu, kwa ajili -yako,ndugu zako na kuachilia
ulinzi wa Damu ya Yesu} mji,anga,ardhi na kwa ajili
ya watu wa mji huo.Hatua ya pili ni kuvaa silaha
[ Efeso.6:13-18 ]Baada ya hayo sasa umfunge mtu
mwenye nguvu-mkuu wa giza(Anga) wa eneo hilo -
[Mathayo. 12:29] kwa kutumia funguo (mamlaka)
uliyopewa na Yesu;ya kufunga na kufungua
[Mathayo. 16:19] .
-Na ndio maana Yesu alitufundisha mbinu za
kufanya ili tuweze kuteka eneo lolote,kupitia kitabu
cha marko.3:27,mathayo 12:29 . “ Hawezi mtu
kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu,na
kuviteka vitu vyake,asipomfunga kwanza yule
mwenye nguvu;ndipo atakapoiteka nyumba yake”.
-Pia Yesu alitupa nguvu ya kufunga na kufungua jambo
lolote la adui.
Mathayo 16:18-19 “Nami nitakupa wewe funguo
za ufalme mbinguni;na lolote utakalolifunga
duniani,litakuwa limefungwa mbinguni;na lolote
utakalolifungua duniani,litakuwa limefunguliwa
mbinguni”.
Pia anasema milango ya kuzimu haitalishinda kanisa
langu.
-Na tayari Bwana alishasema kuwa atatupa sisi
tulio wa uzao wa Ibrahimu kumiliki malango ya Adui
zetu.
Mwanzo 22:17 . “…….na uzao wako utamiliki
mlango wa adui zao”
v Mungu ametuokoa ili tuanze kueneza ufalme wake; na
ili kueneza ufalme wa Mungu ni lazima tuteke miji
na maeneo mbali mbali ili yaweze kuwa chini ya
ufalme wa Mungu.Kwa hiyo kila eneo unalokwenda
ni lazima uliteke na kulimiliki kwa ajili ya ufalme wa
MUNGU.
v Tumezaliwa tuwe washindi na watekaji wa mji
(conquerors)[Rumi.8:37,Mwanzo 24:60,1Yoh. 5:4]
v Kila mahali unapokanyaga, Bwana amekupa wewe
kumiliki.Joshua 1:3
v Pia Yesu ametupa sisi mamlaka ya kukanyaga nge na
nyoka na nguvu zote za yule Adui na hakuna
kitakachotuzuru
Luka .10:19; Rumi. 16:20
- Miji tunayoishi ni lazima ifikie hatua iitwe kwa jina
la Bwana .Eze.45:35- na sio kwa jina la mapepo
kama ilivyokuwa kwa Babeli[Ufunuo.18:2] “…
umeanguka,umeanguka Babeli ule mkuu;umekuwa
maskani ya mashetani,na ngome ya kila roho
mchafu,na kila ndege mchafu mwenye kuchukiza”
-Mji unapokosa maombi unakuwa ni ngome ya
mapepo kama ilivyo kuwa kwa babel.
NB:Mji unapokosa maombi unakuwa kama jalala la kila
aina uchafu wa dhambi.Unajua,mapepo
ninayafananisha na nzi au panya-kwa kawaida
huwezi ukakuta nzi,panya mahali palipo pasafi mara
nyingi utawakuta sehemu chafuchafu kama
jalalani.Wanachofuata inzi ni uchafu na ndivyo
walivyo mapepo na majini.Mahali ambapo maombi
ya toba ya Damu ya Yesu yanafanyika kila siku,sio
rahisi ukute utawala wa shetani.
KANUNI YA MAOMBI HAYA NI:-
· Mathayo 12:29 + Mathayo 16:18-19=mathayo.6:9b-10
KUFUNGA (BINDING).
Tunapozungumzia suala la kufunga, hapa maana
yake ni kama vile unavyomkamata mwizi alafu
ukamfunga miguu na mikono –ndivyo unavyotakiwa
kuwafunga hawa watu wenye nguvu (roho
zitawalazo) mathayo. 12:29.
Tunajua kuwa Yesu alikuja ili kuzivunja kazi za
adui-ibilisi. 1Yohana 3:8
Kufungua (loosing).
Shetani huwa anatabia ya kufunga watu kwa roho za
mauti,magonjwa, uzinzi n.k.Kwa hiyo umepewa
fursa hizo ili uwafungue watu waliofungwa-
isaya.61:1-4.
-Neno la Mungu ni silaha,upanga wa roho.
· Luka 13:11-12, 15-16
· Efeso.6:17b, ebra.4:12
· -Fahamu jambo hili kwenye vita hii unachokiri/
kisema kwa kinywa chako kinakwenda kuwa cha
kwako-ukikiri kushindwa lazima utashindwa
tu. ufunuo.12:11
″ nao wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo na kwa
neno la ushuhuda wao″
Kwa hiyo = NENO + DAMUYA YESU=USHINDI.
Mathayo 4:1-11.
Yesu alimshinda shetani kwa kutumia upanga wa
roho (Neno la Mungu).Kwa hiyo hakikisha kuwa
umejaa neno ndani yako na ulitumie neno kwenye
maombi yako ya kufunga hao watu wenye nguvu.
mathayo. 12:29.
HUU NI MFANO MZURI WA MAOMBI YA KUMFUNGA
MTU MWENYE NGUVU(mfano.Belizebul-
kumfunga belzebuli)
-Kumbuka kabla ya maombi haya hakikisha
umeshafanya toba kama ya Daniel.9 alafu sasa
ujivike silaha za Mungu- Efeso.6:13-18. tamka kwa
kinywa chako mwenyewe kuwa “ninajifunga mshipi
wa kweli kiunoni mwangu kwa jina la Yesu,navaa
drii ya haki kifuani mwangu,najifungia utayari
miguuni mwangu kwa ajili ya injili ya amani,zaidi ya
yote ninatwaa ngao ya imani ambayo kwa hiyo
nitaizima mishale yote yenye moto ya yule
mwovu,napokea chapeo ya wokovu na upanga wa
Roho ambao ni neno la Mungu,nami nadumu katika
sala zote na maombi nikisali kila wakati katika
Roho…”
-Baada ya hapo anza kufunga mkuu wa Anga na
baada ya hapo fanya unachotaka kama ni
kubomoa-bomoa, kuharibu-haribu na
kisha,angamiza n.k.lakini usisahau kujenga na
kupanda kitu,kila unapobomoa na kuharibu na
kuangamiza.
Mfano .umevunja roho ya mauti –hakikisha unatamka
(unapanda)roho ya uzima.[ Yer.1:10,12,Yoh.10:10b]
Huu ni mfano wa maombi haya;
Omba hivi:-
Ninafunga roho ya uchawi iliyokaa katika
Anga kwa minyororo na kwa pingu za chuma
zitokazo mbinguni .Ninasimama katika neno la
Mungu la Math.16:18-19 .ambao unasema “ nami
nitakupa wewe funguo za ufalme wa Mbinguni na
kila utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa
mbinguni- (Math.16:19 ) nami ninakufunga mikono
na miguu kwa jina la Yesu na kwa hilo neno la
BWANA.Nami ninakata kila kiunganishi chochote
kinachounganisha mkuu wa mapepo( rulling spirit-
mkuu wao)na mapepo madogomadogo .Nami
ninakung’oa wewe mkuu wa giza katika anga hili
ninakushusha na kukukanyaga katika jina la
Yesu.Ninalitakasa Anga hili kwa Damu ya Yesu,
nami namkabidhi Roho mtakatifu achukue nafasi ya
kuwa mkuu wa Anga la Eneo(taja jina la eneo
unaloliombea)
- Nami ninavunja roho za zote za ajali, mauti,
uchawi, mafarakano, uzinzi, matambiko na
makafara kwa damu ya Yesu ninateketeza na
kuziharibu kwa jina la Yesu kristo.maana mimi ni
rungu la bwana sawasawa naYeremia 51:20-23
Bwana ameniweka ili kuvunja vunja kazi zako,kama
neno lake linavosema katika - 1Yohana 3:8
“kwamba kwa kusudi hili mwana wa Mungu
alidhihirishwa ili apate kuzivunja kazi zote za ibilisi
shetani “nami kwa Damu Yesu ninavunja kazi zako
zote juu ya maisha yangu,mji huu,biashara
yangu,afya yangu n.k.
-Nami katika jina la Yesu ninajifunika na kujificha
ndani ya damu ya YESU,Ee Mungu ninaomba
unizungushie ukuta wa moto sawaswa na neno lako
la zekaria.2:5. Ninampinga shetani na roho zake
zote za malipizi na visasi alizozikusuda juu yangu
na juu ya ndugu zangu,biashara yangu,masomo
yangu,afya yangu na chochote kilicho chini
yangu;shetani ninakutangazia kuwa huna mamlaka
juu yake kwa jina na kwa Damu ya
YESU.Ninasimamia neno la bwana la
Isaya.54:14-17 linalosema(soma)katika jina la
Yesu nimeomba na kushukuru ameni”
Nb:Huu ni msingi tu wa kukusaidia kuanzia; ila haufungwi
kutumia kanuni nyingine ambazo Roho mtakatifu
atakufundisha kupitia kusoma kwako neno.
MUHIMU:Baada ya Maombi hayo:-
· Omba ulinzi wa Mungu juu yako na juu ya ndugu
zako.
· Vunja roho zote za malipizi na visasi
vinavyokusudiwa na Adui juu ya maisha yako na
ndugu zako
· Soma neno hili - Isaya 54:14-17( ulinzi dhidi ya roho
za malipizi na visasi)[Zekaria 2:5]
-Mshukuru Mungu kwa kuwa ameshajibu maombi yako
katika jina la Yesu.
SHORT SUMMARY.
MFUMO WA MAOMBI YAKO(MTIRIRIKO) UNATAKIWA
UWE HIVI:-
A.Toba ya Damu ya Yesu – Isa.1:18,43:25
· Tubu kwa ajili ya ndugu zako,wewe mwenyewe
marafiki na watu wote wa karibu yako,omba ulinzi
kwa ajili yako na ndugu zako.
· Tubu kwa ajili ya Mji wako,Anga lake ,Ardhi n.k.
takasa na umwage Damu ya Yesu ya ulinzi ya
kufunika Anga,Mji,Ardhi,Barabara,maji n.k
B.KUOMBEA MJI,KANISA FAMILIA N.K
-Tumia funguo za Mathayo 16:19,18:18 funga wakuu wa
giza ,Anga na mapepo wabaya kwenye Anga n.k
Wasete kuzimu kwa jina na kwa Damu ya YESU.
-kata kila connection(kiunganishi) inayowaunganisha
wakuu wa giza na mapepo wadogowadogo.
-vunja kazi za ibilisi [1Yohana3:8,Yeremia
51:20-23]
C.HITIMISHO.
Ulinzi juu yako, ndugu zako ,vunja roho ya malipizi na
visasi- Isa.54:14 17 . “……watu watakaokusanyana
juu yako wataanguka……….kila silaha
itakayofanyika juu yako haitafanikiwa…..”
Nb:Kama bado maneno hayo yote ya biblia hayajakaa
kichwani,basi hakikisha unakuwa na biblia karibu;
kila unapofanya maombi yako ya aina hii.
Neno la Mwisho.
Maombi yako ni ya muhimu sana kwa ajili ya
huduma hii kuendelea kusonga
mbele.philip.3:13-14 . “ Ndugu sijidhanii nafsi yangu
kwamba nimekwisha kushika ila natenda neno moja
tu;…nikiyachuchumilia yaliyo mbele;nakaza
mwendo nifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu
wa Mungu katika kristo Yesu.
PAST.loy

Maoni 0:
Chapisha Maoni
Welcome
Jisajili kwenye Chapisha Maoni [Atom]
<< Nyumbani