REVIVAL BUILDERS CHURCH
BUILDERS OF GOD'S KINGDOMS, Tunajenga ufalme wa Mungu,Yunakuinua umjue Mungu binafsi,Tunainua uamsho mkuu wa , Maombi,MIUJIZA,na wokovu+WEWE NI SEHEMU YA UAMSHO WA SIKU ZA MWISHO, KUWA SABABU, KUWA UAMSHO
Jumanne, 18 Oktoba 2022
Ijumaa, 14 Oktoba 2022
SABABU YA ISRAEL KUUTOINGIA KANANI.
Tunaona baada ya israel kutolewa misri walikuwa na safari ambayo lengo lake wafike kanani lkn tunaona hawakuweza kuingia baadhi yao kwa sababu mbalimbali kama tutakavyoona mbeleni na kama tunavyoona sisi ndiyo israel kiroho na tumetoka misri yaani dhambini na shetani ndiye alikuwa mtesi wetu sasa tunawe kuona kuwa rohoni sisi ni israel wa kiroho maana tunakuwa wazao wa ibrahim kwa imani. garati 3:7-9. "walio wa imani ndio wana wa ibrahim"
sasa waweza ona MUNGU amewafanya mataifa kuwa wana wa ibrahimu;na ibrahim ndiye baba yake israel hivyo mataifa wamepata haki hii kupitia kristo kwa imani. sasa tunapokuwa tunaongea juu ya sababu zilizowakosesha nasi tujue inawezekana tunafanya hayohayo yaliyowakosesha wenzetu. hivyo yafaa kujiadhari tusije ikosa kanani ya mbinguni 1korth 10:1-12; niajabu sana tambua haya ni mambo yakujitazia au kujiangalizia ili nawe usije ukatenda hayohayo ukaangamia "maana ajizaniae amesimama aangalie asianguke"
nitaendelea na sababu ...
sababu ya kwanza kabisa ni
1*****KUSAHAU MATENDO YA MUNGU ALIYOWAYENDEA KWA HARAKA.*******
Wengi wao walipita ktk bahari ya shamu kimiujiza baada ya kuona wamisri walio wafuatia wamepigwa kwa maji na kuangamia waliimba sana wakiongozwa na miriam lkn baada ya muda mfupi walikuwawamesahau na wakaanza kumchukiza MUNGU,kana kwamba hawakuona matendo ya Mungu yalivyo makuu ktk maisha yao. hili ni mafano kwetu kama wengi wetu wafanyavyo. mfano unaweza kumwona mtu ni dhaifu hawezi kufanya lolote lkn anakuja kwa Yesu anaponywa lkn baada ya kuponywa anasahau kuwa alitaka kufa na aliyempa uzima ni Yesu utamwona amwona ameanza kushirikiana na shetani kwa kufanya matendo yaliyochukizo .mf ulevi na uasherati.
2****KUSHINDWA KUMNGOJA MUNGU NA SHAURI LAKE.*****-
Wengi wa watu hawa walikosa tunda la uvumilivu na wakawa watu ambao wakiona hali ambayo inawapa shida ni kupiga kelele;ingawa walijua kuwa MUNGU anatenda kila anapoitwa lkn wao hawakuvumilia kabisa . sawa na miongini mwetu mtu anajua kabisa tatizo alilonalo linatiba itokayo kwa BWANA lkn akiona kama kuchelewa anachepuka njia na kumfuata mashauri yake mwenyewe. siku zote Mungu hatembei kwa mashauri/mawazo yetu kumbuka mawazo ya MUNGU sio mawazo yetu.
pia tambua hili ujue ukamrudie BWANA . Mungu hatembei kwa majira yetu lkn sisi lazima tutembee kwa wakati wa MUNGU ;Si vizuri kanisa la Mungu kuishi kwa majira na wakati wake lenyewe lazima tuishi kwa wakati wa MUNGU. Watu wanaotaka kutembea kwa wakati wao ndio tunasikia wanasema Mungu amechelewa,hasikii,haoni ama amenyamaza. Mungu hachelewi wala hawahi hivyo ni vizuri kutembea kwa wakati wa MUNGU ili usije ukamwona Mungu hasikii.
YAMEKUWA MAFANO KWETU...
1KORTH 10:1-12.
biblia inasema wote walibatizwa ktk wingu wawe wa Musa.......wote walinywea mwamba wa roho...lkn wengi wao hawakuweza kuingia kwa kuwa Mungu hakupendezwa nao..
na mambo hayo yaliandikwa ili kutuonya sisi zamani hizi"
Ni jambo la kusikitisha sana kwa watu kikionja kipawa cha Mungu cha roho kushindwa kuingia mbinguni; mara nyingi tunataliwa kuelewa kuwa sio kila aliyeanza safari anaweza kuimaliza lahasha wengine wanafia na kuishia njiani. Ina maana hivi kuna namna Mungu anataka ili tumalize safari yetu na tukishindwa kuifuata tusitazamie kumaliza hapo lazima shetani atapata tu wafuasi wa kumfuata na kufanya wengi wao kubadili nia ya awali na hatimae kuangamia kwa kuacha njia ya haki.
tuendelee na sababu
zaburi 106:10-43:
3*****KUMJARIBU MUNGU.
Kumjaribu Mungu ni kufanya jammbo makusudi ili uone kama Mungu atalofanya au atakusaidia mafano math 4:6-7 "ikiwa ndiwe mwana wa Mungu jitupe chini..........Yesu akamwambia imeandikwa usimjaribu Mungu wako"
unaweza ona hapa shetani ataka Yesu ajitupe makusudi ili aone kama utamwokoa" si vizuri kusanya kitu cha makusudi ili uone atakachofanya .
Biblia inatueleza wazi kuwa wana wa israel walikuwa watu wenye nia ambazo zilimchukiza sana Mungu kwa maisha yao walipofika huko jangwani kumjaribu MUNGU huko masa. ni vizuri kutofanya mambo kwa nia hii isiyofaa.
wewe waweza kujiuliza je humjaribu Mungu ktk mambo unayoyafanya ? Ni vema tusiwe watu wasio na nia kama hii maana hao walishindwa kuingia kwa kumjaribu tu MUNGU.
4*****KUMHUSUDU MUSA NA HARUNI. hes 16:1-19.
Kuhusudu maana yake kuwa kinyume naye. hapa tunaona dathan na kora,abiramu na watu wrngine walianza kubishana na kushawishi watu kuwa kinyume na MUSA ukisoma musa anawauliza je nanyi mwataka ukuhani?
hapa lazima tujue kitu ambacho kimewavaa watu wengi kupenda ukuu;usitafute mambo haya utashindwa kumwona MUNGU mbinguni. yer 45:1-5. "je unajitafutia mambo makuu? usiyatafute...usiyasafute mambo hayo kwani hayo ni chanzo cha ugomvi baina ya watu wengi ktk ulimwengu huu. kanisa lazima kujihadhari na roho hii ni tusije tukakosa kanani yetu ya mbinguni tukumbuke kuwa mambo haya ni mfano kwetu ikiwa tukayafanya kama ya kora na wenzake basi tujue mbinguni hatutaenda kabisa.
nitaendelea























