Alhamisi, 30 Juni 2016

CHANZO CHA UCHUNGU.


Bwana Yesu Asifiwe Sana Wana Wa Mungu.

Watu Wengi Wamepata Shida Kubwa Sana Kwenye Maisha Yao Kwa Kuishi Na Uchungu Na Hata Umewaletea Madhara Makubwa Kiafya Bila Sababu .

Lkn Leo Nataka Nikueleze Kifupi Kuhusu Sababu Hasa Ya Uchungu.

EBRANIA 12:14-15

TAFUTENI KWA BIDII KUWA NA AMANI NA WATU WOTE,NA HUO UTAKATIFU -....,15 MKIANGALIA SANA SANA SANA NEEMA YA MUNGU ASIIPUNGUKIE NEEMA YA MUNGU;SHINA LA UCHUNGU LISIJE LIKACHIPUKA NA KUWASUMBUA ..,

angalia mst15  utaona kuwa chanzo cha uchungu wa watu wengi ni KUPUNGUKIWA NEEMA, Yaani Maisha Yako Yanakosa Viwango Vya Kiroho, Na Kushindwa Kukaa Chini Ya Roho Mtakatifu.

Kwa Sababu Ya Kukosa Kuongozwa Roho Wa Mungu Watu Wengi Wamekuwa Na Mambo Haya-

1=kushindwa Kusamehe.

2=kutokusahau Walio Waumiza,

3=kubeba Kisasi.

4=kuona Anaonewa Kwa Kila Analotenda/anatendewa.

Hii Imeleta Hasira Imbayo Imekuwa Kama Sumu Isiyoisha Ndani Ya Watu Na Kusabisha Maumivu Makubwa Ktk Mioyo Yao,

Watu wengi kwa kuendelea kuacha su hii mioyoni mwao imewalete bp hata kuwaletea mauti ya kiroho na kimwili.

Ikumbukwe kutosamehe, ni moja ya mambo yanayoleta MUNGU kutokusikia hata maombi yako. maana imeandikwa usiposamehe Mungu hatakusamehe pia.

NAMNA YA KUSHINDA UCHUNGU

1-KUSAMEHE NA KUACHILIA.
Kusamehe ni kutangaza msamaha na kuachilia ni ile hali ya kutohesabu hatia tena aliyekukosea na hii huambatana na kusahau kabisa uliyotendewa na mtu huyo. math 6:14-15

2: KUOMBA MAOMBI YA TOBA.
>KUOMBA TOBA MWENYEWE.

Kumbuka matokeo ya kuchipuka au kuota kwa uchungu ni kupungukiwa neema sasa neema haipungui tu ila unakuwa umeshindwa kuishi ktk viwango vya utakatifu na MUNGU wako  kwa hiyo ni lazima uombe rehema ili urudi kwenye njia. yaani kile kiwango cha neema kiwe ktk hali yake ndipo uchungu utatoka ktk moyo wako. yakobo  1:5   "Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa hekima na aombe dua kwa Mungu"

3..KUBALI KUNYENYEKEA NA KUTII.

Matokeo ya kupungukiwa neema ni jibu la kukosa kunyenyekea.
biblia inasema  "  lakini MUNGU hutujalia neema iliyozidi;kwa hiyo husema,Mungu huwapinga wajikuzao bali huwapa neema wanyenyekevu"   yakobo 4:6.

kinachowafanya wengi kuishi kwa uchungu ni kule kukubali kunyenyekea na lulitii neno la MUNGU wengi hawataki kifuata hata ushauri watumishi wa MUNGU na neno .wamejihesabia haki hawataki kufuata maelezo hii imewaletea uharibifu wa haraka na kupotea kwa kichua maamuzi yasiyostahili..

Na ili uweze kwenda ktk njia njema na kuponywa na hili rudi ktk utii na neema itarudishwa mdani yako na hii ndio dawa hasa ya kupona kidonda hiki cha moyo wako.

Ni Vema Kutambua Hili  Na Mungu Akusaidie Kushinda Uchungu.

MUNGU AKUPE NGUVU YA KUVUKA KTK JAMBO HILI

MAWASILIANO.

NA MAOMBEZI.
0766891120