ELIMU/MAFUNDISHO YA MASHETANI.
Bwana YESU Asifiwe wana wa MUNGU leo imempendeza BWANA kujifunza somo hili linalohusu mafundisho ya mashetani.
NINI MAANA YA ELIMU/MAFUNDISHO YA MASHETANI?
Mafundisho ya mashetani ni mafundisho yanayofundishwa kinyume na mafundisho ya kweli ya kristo. Walimu wanaofundisha haya wanafundisha kinyume na injili ya kweli na huonesha wazi wazi kuwa kristo bado hajatutoa dhambini yaani hutufanya tujione bado sisi tuaminio hatujaamini au yanaonesha kazi ya msalaba kuea haijakamilika bado. 1timotheo 4:1-4 " "
Biblia inasema siku za mwisho watu watajitenga na imani ya kweli na kufuata mafundisho ya mashetani na biblia inaposema mafundisho ya mashetanihaimanishi kuwashetani au mashetani yanakuja yenyewe kufundisha bali yana watu wanaofanya kazi hiyo. Kumbuka watu hujigeuza yaani wamejifanya kama watumishi watakatifu wa Mungu aliyehai..kumbuka watumishi wa ibilisi hujigeuza wafanane na watumishi wa kweli sio kwamba ndivyo walivyo bali wamejigeuza tu wawe mfano wa watumishi wa kweli ila sio halisia.
CHANZO CHA MAFUNDISHO YA MASHETANI
Mafundisho haya yanatokana na vyanzo hivi vifuatavyo.
1…Chanzo kwanza kabisa ni ROHO ZIDANGANYAZO 1timoth 4:1
" Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati
za mwisho wengine watajitenga na imani,
wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya
mashetani;
Roho hizi wakati mwingine huitwa roho mbaya na hii roho zina uvuvio wa pepo wachafu..kumbuka kuwa
"Roho ina uwezo wa kumsemesha mtu na kumwaminisha juu ya jambo fulani.Na kumfanya mtu aamini vilevile;
roho hizi ndizo hufanya kazi ya kutoa utabili wa uongo na huweza kuja kwa ndoto maono au kukusememesha kimya kimya. yoh 8:43... .
8:43
" Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba
yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa
mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika
kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake.
Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe;
kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.
biblia inatueleza kuwa shetani ndiye mwanzilishi wa uongo na ndiye baba wa huo kwa hiyo utambue roho yake hufanya hayohayo, mhimu ujue hivi roho ya ibilisi hufanya uvuvio juu ya watu wake na huyatetanda mambo yao kwa nguvu ya huyo bila wao kujua..
NITAENDELEA
