Ijumaa, 8 Mei 2015

AGANO

kusoma sehemu ya 3 na 4 ya somo hili
wiki iliyopita basi BONYEZA HAPA kabla
hujaendelea na sehemu ya 5 na 6. Barikiwa
SEMINA YA MWL MWAKASEGE DODOMA
SOMO: FAIDA ZA KUTEMBEA KATIKA BARAKA ZA
AGANO NA MUNGU.
Neno kuu: Eph 1:3
DAY FIVE.
Utangulizi: Luk 22:20, Ebr 8:6
•Maana ya Bora( agano): lenye uepesi wa kutumia
agano ili kufikia kusudi la agano lililowekwa. Math
5:17-19, Ebr 8:7,13
•Maana ya kuukuu: matokeo ya kitu kutoweza
kuhimili matumizi. Inaweza kusababishwa na:
•Ongezeko la matumizi bila kupumzishwa/
Matumizi ya mara kwa mara
•Cha zamani hakiendani na hali ya wakati wa sasa.
•Kuna uhusiano kati ya agano jipya na maagano
yaliyopita.
•Agano jipya limekuja kuyakakamilisha maagano
yaliyopita. Ndani yake limebeba upatikanaji wa
maagano yaluyotangulia.
•Huwezi pata maagano yaliyopita bila agano jipya.
CHANGAMOTO TULIZONAZO LEO
1. Kutoyatazama maagano yaliyotangulia kwa jicho
la agano jipya.
2. Kutokujua namna ya kutumia kilichopo ndani ya
agano jipya ili kupata yale yaliyomo katika
maagano yaliyotangulia
Agano la Ibrahim
Gal 3:13,14,29
Baraka ya Ibrahim na ahadi alizohaidiwa.
Mwa 24:1,34,35
•Alibarikiwa katika vitu vyote.
Mwa 12:2, 22:17
Kumiliki lango la adui wako. Mwa 15:18-19
•Haiwezekani uzao wake kutomiliki aridhi/ nchi.
Rom 4:13. Hii ni ahadi ya Ibrahim.
Agano la Sinai
Gal 3:13-14.
•Kristo alikufa msalabani ili tuipate baraka ya
Ibrahim.
Gal 3:16-29
•Kilichopatikana katika agano hili ni kutengenezwa
kwa hema ili Mungu apate maskani.
•Mungu alikuwa akiachilia ufalme wake kwa
wanadamu.
•Ndani ya sheria kukatokea ukuhani au agano la
Lawi.
•Wazaliwa wa kwanza kupata heshima yao.
Chakula cha Bwana ni sehemu ya agano. Luk
1:31-32, Ufu 3:21.
Agano la Daudi
•Mungu aliteremsha kiti cha Mfalme.
•Yerusalem ni mji wa Mfalme mkuu.
Agano la Jerusalem
•Mungu anaweka hekima kwa wanadamu kusema
juu ya Yerusalem. Mwa 6:18.
DAY SIX
Utangulizi:
Swali: Unazipataje hizo baraka za agano?
Gal 3:13-14
•Kazi ya msalaba ni kutoa nafasi kwa watu wasio
wayahudi( mataifa) kupata baraka na ahadi ya
Ibrahim kupitia Kristo.
Rom 8:16-17, Gal 3:29
•Ukitaka kurithi baraka za Ibrahim ni lazima uwe
mrithi wake
HATUA ZA KUKUSAIDIA KUONA BARAKA
ZINATOKEA KATIKA MAISHA YAKO NA
UNATEMBEA NAZO.
1. Zaliwa mara ya pili ili uwe mwana wa Mungu.
Eph1:3, 4,5,11,13,14
2Cor 5: 17, Yoh 3:3
•Sisi tulio wa mataifa ni lazima tuzaliwe mara ya
pili ili tuwe warithi wa Ibrahim.
•Kama haujaokoka ni lazima uokoke.
2. Fahamu ya kuwa kwakuwa wewe ni mwana wa
Mungu ni mrithi pamoja na Kristo.
Gal 4:6-7, Rom 8:16-17, Luk 15:11-32
•Ili upokee baraka ni lazima ujue ya kuwa wewe ni
mrithi. Eph 1:13-14
•Kazi ya Roho mtakatifu ni kutushuhudia.
3. Omba maombi yanayohusu urithi wako.
•Mungu akujulishe na kukuonesha urithi ulionao.
Efe 1:17-18
Tujue utajiri wa utukufu wa urithi wake katika
watakatifu wake.
•Ufalme wa mbinguni ni urithi wako. Math 25:34
•Uzima wa milele ni urithi wako. Math 19:29
•Baraka ndani ya ndoa. 1Pet 3:7-9
•Wenye hekima kurithi utukufu. Mith 3:35
•Mbinguni ni urithi. 1Cor 15:50-56
•Malaika kukuhudumia ni urithi wako. Ebr 1:14
•Jina la Yesu ni urithi wetu. 2Nya 7:14
•Aridhi ni urithi wetu. Kuna mahali Mungu
amekupangia kurithi. Ebr 11:8
•Omba akupe huo urithi uwe wako. Mdo 20:32, Zab
2:7-8
4. Ukue katika Kristo usibaki mtoto. Gal 4:1-3, Col
1:13
•Uaminifu
Luk 16:10-12
Usipokuwa mwaminifu Mungu alipokupa kufanya
huduma na mtu mwingine hutapewa huduma yako
mwenyewe.
Mith 28:20, Mith 23:7, 1Cor 13:11, 3:1-9, Yoh 15:15,
Ayu 22:21, Zab 133:1-3, Efe 4:11
Litaendelea…..

Jumanne, 5 Mei 2015

JINSI YA KUFANYA MAONO YAWE HAI


Bila ya kuwa na maono ya wapi unaelekea ni rahisi
kuchukuliwa na upepo na kupelekwa
usikokutazamia. Maono yatakufanya ujue ni nini
ufanye kwa ajili ya Mungu na maisha yako kwa
ujumla.
Mithali 29: 18 Pasipo maono, watu huacha kujizuia;
Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
Maono yako kwa ajili ya kazi ya Mungu ni lazima
yaendane na agizo kuu alilolitoa Bwana Yesu kwa
wote wanaomwamini.
Marko 16:15 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni
mwote, mkaihubiri injili kwa kila kiumbe.
Ni lazima mara zote agizo hili liwe ndani yako ili
unapoendelea na maono yako usijeenda mbali na
agizo hili.
Shetani hujaribu kuyafisha maono yako na
usipokuwa mwangalifu atayapoteza kabisa. Yeye
mara zote hutaka kituzuia kuyafanya mapenzi ya
Mungu, anajua akiyaua maono yetu hatutaweza
kuifanya kazi ya Mungu kwa ukamilifu.
2Korintho 2:11 Shetani asije akapata kutushinda;
kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.
Mambo yafuatayo shetani huyatumia kuua maono
yetu:
1. Dhambi ambazo hazijatubiwa
Isaya 59:9-12 Mistari hii inaonyesha kuwa dhambi
isipotubiwa hupofusha macho ya rohoni hivyo
hutaweza kuyaona maono yako. Dhambi inakuweka
mbali na utukufu wa Mungu.
2. Uhusiano uliovinjika katika mwili wa Kristo
Tunaporuhusu makosa ya ndugu zetu katika Kristo
kuzaa uchungu badala ya kusamehe, tunaruhusu
shetani kuyafunga macho yetu ya kiroho na hivyo
kushindwa kuiona njia ya kuelekea kwenye maono
yetu.
3. Tamaa ya mambo yanayoonekana
Zaburi 119:37 Unigeuze macho yangu nisitazame
yasiyofaa, unihuishe katika njia yako.
Ukiangalia sana mambo ya dunia na tamaa zake
utajikuta unayasahau maono yako na kubaki
umefungwa na mambo hayo.
4. Kuangalia sana mambo ya nyuma.
Unapoacha kutazama mbele unapoelekea na
kuweka nguvu na akili yako yote katika mambo ya
nyuma yaliyopita, utapoteza kusudi lako na maono
yako.
Mwanzo 19:26 Lakini mkewe Lutu akatazama
nyuma yake, akawa nguzo ya chumvi.
Wafilipi 3:13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba
nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu;
nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo
mbele.
5. Kutumia muda mwingi kuangalia matatizo
Shetani hujaribu kutufanya tuangalie tu matatizo
tuliyonayo na yale yanayoweza kutokea
tunapoyafanyia kazi maono yetu hivyo kutuondolea
imani ya kuyakamilisha. Biblia katika kitabu cha
hesabu inaelezea habari za wapelelezi kumi
waliorudi na habari za kukatisha tamaa katika
kuiendea nchi ya ahadi maana waliangalia zaidi
matatizo na kupoteza maono yao ya kuingia nchi ya
ahadi.
Joshua na Kaleb waliona zaidi ya matatizo,
waliuona ukuu na uaminifu wa Mungu. Hawakuwa
na hofu yoyote hivyo waliweza kuingia nchi ya
ahadi (kukamilisha maono yao) maana walimwamini
Mungu. Petro alijaribu kutembea juu ya maji lakini
alipoona mawimbi akasahau Yesu aliyekuwa mbele
yake akimwambia njoo, akaweka akili kwenye
mawimbi akaanza kuzama.
Ili tuweze kuyafanikisha maono yetu ni lazima tuwe
na uhusiano na ushirika wa karibu na Roho
Mtakatifu.
Ubarikiwe na BWANA Yesu.