Jumanne, 18 Oktoba 2022

UAMSHO RUVUMA


 










Ijumaa, 14 Oktoba 2022

SABABU YA ISRAEL KUUTOINGIA KANANI.


Wana wa israel ni taifa teule la MUNGU; Ni watu ambao walikuwa wameteuliwa na Mungu ili wamwakilishe duniani ;na Mungu alikuwa amefanya maagano na taifa hili na akalichukulia kama mazao wake wa pekee;tunaona mbingu/serikali ya MUNGU wa mbinguni ilikuwa ikiwakilisha na israel.

Tunaona baada ya israel kutolewa misri walikuwa na safari ambayo lengo lake wafike kanani lkn tunaona hawakuweza kuingia baadhi yao kwa sababu mbalimbali kama tutakavyoona mbeleni na kama tunavyoona sisi ndiyo israel kiroho na tumetoka misri yaani dhambini na shetani ndiye alikuwa mtesi wetu sasa tunawe kuona kuwa rohoni sisi ni israel wa kiroho maana tunakuwa wazao wa ibrahim kwa imani. garati 3:7-9. "walio wa imani ndio wana wa ibrahim"
sasa waweza ona MUNGU amewafanya mataifa kuwa wana wa ibrahimu;na ibrahim ndiye baba yake israel hivyo mataifa wamepata haki hii kupitia kristo kwa imani. sasa tunapokuwa tunaongea juu ya sababu zilizowakosesha nasi tujue inawezekana tunafanya hayohayo yaliyowakosesha wenzetu. hivyo yafaa kujiadhari tusije ikosa kanani ya mbinguni 1korth 10:1-12;  niajabu sana tambua haya ni mambo yakujitazia au kujiangalizia ili nawe usije ukatenda hayohayo ukaangamia "maana ajizaniae amesimama aangalie asianguke"

nitaendelea na sababu ...

sababu ya kwanza kabisa ni
1*****KUSAHAU MATENDO YA MUNGU ALIYOWAYENDEA KWA HARAKA.*******

Wengi wao walipita ktk bahari ya shamu kimiujiza baada ya kuona wamisri walio wafuatia wamepigwa kwa maji na kuangamia waliimba sana wakiongozwa na miriam lkn baada ya muda mfupi walikuwawamesahau na wakaanza kumchukiza MUNGU,kana kwamba hawakuona matendo ya Mungu yalivyo makuu ktk maisha yao. hili ni mafano kwetu kama wengi wetu wafanyavyo. mfano unaweza kumwona mtu ni dhaifu hawezi kufanya lolote lkn anakuja kwa Yesu anaponywa lkn baada ya kuponywa anasahau kuwa alitaka kufa na aliyempa uzima ni Yesu utamwona amwona ameanza kushirikiana na shetani kwa kufanya matendo yaliyochukizo .mf ulevi na uasherati.

2****KUSHINDWA KUMNGOJA MUNGU NA SHAURI LAKE.*****-

Wengi wa watu hawa walikosa tunda la uvumilivu na wakawa watu ambao wakiona hali ambayo inawapa shida ni kupiga kelele;ingawa walijua kuwa MUNGU anatenda kila anapoitwa lkn wao hawakuvumilia kabisa . sawa na miongini mwetu mtu anajua kabisa tatizo alilonalo linatiba itokayo kwa BWANA lkn akiona kama kuchelewa anachepuka njia na kumfuata mashauri yake mwenyewe. siku zote Mungu hatembei kwa mashauri/mawazo yetu kumbuka mawazo ya MUNGU sio mawazo yetu.

pia tambua hili ujue ukamrudie BWANA . Mungu hatembei kwa majira yetu lkn sisi lazima tutembee kwa wakati wa MUNGU ;Si vizuri kanisa la Mungu kuishi kwa majira na wakati wake lenyewe lazima tuishi kwa wakati wa MUNGU. Watu wanaotaka kutembea kwa wakati wao ndio tunasikia wanasema Mungu amechelewa,hasikii,haoni ama amenyamaza. Mungu hachelewi wala hawahi hivyo ni vizuri kutembea kwa wakati wa MUNGU ili usije ukamwona Mungu hasikii.

YAMEKUWA MAFANO KWETU...

1KORTH 10:1-12.
biblia inasema wote walibatizwa ktk wingu wawe wa Musa.......wote walinywea mwamba wa roho...lkn wengi wao hawakuweza kuingia kwa kuwa Mungu hakupendezwa nao..
na mambo hayo yaliandikwa ili kutuonya sisi zamani hizi"   

Ni jambo la kusikitisha sana kwa watu kikionja kipawa cha Mungu cha roho kushindwa kuingia mbinguni; mara nyingi tunataliwa kuelewa kuwa sio kila aliyeanza safari anaweza kuimaliza lahasha wengine wanafia na kuishia njiani. Ina maana hivi kuna namna Mungu anataka ili tumalize safari yetu na tukishindwa kuifuata tusitazamie kumaliza hapo lazima shetani atapata tu wafuasi wa kumfuata na kufanya wengi wao kubadili nia ya awali na hatimae kuangamia kwa kuacha njia ya haki.
tuendelee na sababu
zaburi 106:10-43:

3*****KUMJARIBU MUNGU.
Kumjaribu Mungu ni kufanya jammbo makusudi ili uone kama Mungu atalofanya au atakusaidia mafano math 4:6-7  "ikiwa ndiwe mwana wa Mungu jitupe chini..........Yesu akamwambia imeandikwa usimjaribu Mungu wako"
unaweza ona hapa shetani ataka Yesu ajitupe makusudi ili aone kama utamwokoa" si vizuri kusanya kitu cha makusudi ili uone atakachofanya .

Biblia inatueleza wazi kuwa wana wa israel walikuwa watu wenye nia ambazo zilimchukiza sana Mungu kwa maisha yao walipofika huko jangwani kumjaribu MUNGU huko masa. ni vizuri kutofanya mambo kwa nia hii isiyofaa.

wewe waweza kujiuliza je humjaribu Mungu ktk mambo unayoyafanya ? Ni vema tusiwe watu wasio na nia kama hii maana hao walishindwa kuingia kwa kumjaribu tu MUNGU.

4*****KUMHUSUDU MUSA NA HARUNI. hes 16:1-19.
Kuhusudu maana yake kuwa kinyume naye. hapa tunaona dathan na kora,abiramu na watu wrngine walianza kubishana na kushawishi watu kuwa kinyume na MUSA ukisoma musa anawauliza je nanyi mwataka ukuhani?

hapa lazima tujue kitu ambacho kimewavaa watu wengi kupenda ukuu;usitafute mambo haya utashindwa kumwona MUNGU mbinguni. yer 45:1-5.  "je unajitafutia mambo makuu? usiyatafute...usiyasafute mambo hayo kwani hayo ni chanzo cha ugomvi baina ya watu wengi ktk ulimwengu huu. kanisa lazima kujihadhari na roho hii ni tusije tukakosa kanani yetu ya mbinguni  tukumbuke kuwa mambo haya ni mfano kwetu ikiwa tukayafanya kama ya kora na wenzake basi tujue mbinguni hatutaenda kabisa.

nitaendelea

Jumatano, 1 Februari 2017

MKE NI MBEBA HUDUMA YA MME

Unaweza usinielewe kirahisi lkn mke ni mtu anasabisha huduma ya mme kupata kibali zaidi kuliko kwanza, MITH 18:22"APATAYE MKE APATA KITU CHEMA;NAYE AJIPATIA KIBALI MBELE ZA BWANA"

Usimzalau mkeo ;usimfanye mkeo mtumwa wako,mpe nafasi uone jinsi utakavyofanikiwa ktk utumishi wako.

kama hajajua mengi kuhusu utumishi jifunze kumfundisha na kumjenga ili awe chombo cha BWANA na aweze kuwa mtu wa kwanza kukufanya utoke mahali ukipo na kufika mahali pa juu.


Ukitaka kujua ebu fikiri ukichokoza mke wako na kutoelewana naye unazuia majibu ya maombi yako.


Mke ni msaidizi wa mme sasa jiulize anasaidia nini.lkn ufikiri pia kusudi la kuumbwa ni nini. ukijua ndipo utajua kwa nini Mungu anasema si vema mwanaume awe peke yake.

Kwa maana nyingine ni kwamba wajibu aliopewa adamu si vema aufanye mwenyewe ila lazima awepo na eva.

mskusudi mawili ya MUNGU ya kuumba ni


1-kutunza bustani.

2-kumwabudu.

Usipotimiza haya unakuwa bado hujatimiza wajibu wako sawasawa kwa Mungu.

Sifunze kumfundisha mkeo kukubeba kihuduma yako ili ufanikiwe

Lebo:

USIJIANGAMIZE MWENYEWE

Haleluya wana MUNGU ninayofuraha kubwa kukuletea ujumbe huu siku ya leo.

Yakobo. 3:2-14.
Mara nyingi watu tunahitaji sana kufanikiwa na kufika mahali tunapotoka lkn ipo shida ambayo ipo kwetu inasumbua na kutufanya tushindwe kufika tutakako. Shida kubwa inayotufelisha na ukiri wetu ktk kinywa(Ulimi)
Ni rahisi kujua unatakiwa ujue ulimi nini na unasehemu gani ktk mambo uliyokusudia kwenye maisha:-)
ULIMI NI SAWA NA USUKANI.
Usukani unaelekeza chombo kikubwa ktk mwelekeo anaotaka dreva,sasa wewe ndie dreva ila ulimi ni usukani wa mwili wako,maisha yako.
Sikia ni kwamba unatakia ufahamu kuwa unachotaka au unakotaka kufika lazima ulimi/usemi wako unene kama matakwa au nia yako ilivyo,huwezi fika unataka kwenda wakati kinywa au usemi wako unanena tofauti, ok ni jambo rahisi tu, Yesu anatuambia kuwa kila mtakalolifunga duniani limefungwa mbinguni, sasa hatufungi kimya,tunafunga kwa kunena,unahitaji usema il i yatokee, jambo lolote ktk ulimwengu wa roho haliji ktk ulimwengu wa mwili mpaka umelisemea ulimwengu huu ukatii na kuruhusu, ok kumbe kinywa chako kinauleta ulimwengu wa roho ktk ulimwengu wa mwili,ni rahisi tu kuelewa biblia inasema ulimi ndio huleta laana au baraka mst wa 10*
KUMBE...,mwelekeza laana au baraka ni ulimi/kinywa chako.
Kifo/mauti ya mafanikio yako,ndoa yako,na familia yako ipo ulimini mwako.
Mith 18:20-21a
."Mauti na uzima huwa ktk uwezo ktk uwezo wa ulimi."
Kumbe uwezo wa kufanikiwa au kushindwa ni vile wewe unaweza kutamka juu ya jambo fulani, mst wa 20*unasema tumbo hujazwa matunda ya kinywa, matokeo ya kusema kwako ndio mfumo utakaoishi .
ULIMI NI MOTO.yakobo 3:6
Ulimi ndio chanzo cha uharibifu mkubwa, tafakari moto unaweza kuwa mdogo ukasababisha msitu mkubwa ukawaka na kuteketea, msitu wa mambo yako makubwa,unaweza ukauangamiza kwa sekunde tu, hili litatokea ukiamua kuyasemea vibaya, maono yako yanaweza kufa kwa kuamua kuyatamkia vibaya,watendakazi kwenye huduma yako wanaweza kuharibika kwa kuwatamkia uharibifu. Makanisa mengi yanashindwa kufanikiwa shida ni kuwasemea wanaowaongoza laana.
Mungu aliponifundisha nilibidi nibadili jinsi ya kuongea na walionyuma yangu kwani ningezuia mfumo wa mafanikio ya huduma yangu, usikubali kuwasha moto mbaya kwa ulimi wako, jifunze kutumia maneno yako vizuri,tumia ulimi wako kujishibisha mema,.
UBALIKIWE

Lebo:

Alhamisi, 30 Juni 2016

CHANZO CHA UCHUNGU.


Bwana Yesu Asifiwe Sana Wana Wa Mungu.

Watu Wengi Wamepata Shida Kubwa Sana Kwenye Maisha Yao Kwa Kuishi Na Uchungu Na Hata Umewaletea Madhara Makubwa Kiafya Bila Sababu .

Lkn Leo Nataka Nikueleze Kifupi Kuhusu Sababu Hasa Ya Uchungu.

EBRANIA 12:14-15

TAFUTENI KWA BIDII KUWA NA AMANI NA WATU WOTE,NA HUO UTAKATIFU -....,15 MKIANGALIA SANA SANA SANA NEEMA YA MUNGU ASIIPUNGUKIE NEEMA YA MUNGU;SHINA LA UCHUNGU LISIJE LIKACHIPUKA NA KUWASUMBUA ..,

angalia mst15  utaona kuwa chanzo cha uchungu wa watu wengi ni KUPUNGUKIWA NEEMA, Yaani Maisha Yako Yanakosa Viwango Vya Kiroho, Na Kushindwa Kukaa Chini Ya Roho Mtakatifu.

Kwa Sababu Ya Kukosa Kuongozwa Roho Wa Mungu Watu Wengi Wamekuwa Na Mambo Haya-

1=kushindwa Kusamehe.

2=kutokusahau Walio Waumiza,

3=kubeba Kisasi.

4=kuona Anaonewa Kwa Kila Analotenda/anatendewa.

Hii Imeleta Hasira Imbayo Imekuwa Kama Sumu Isiyoisha Ndani Ya Watu Na Kusabisha Maumivu Makubwa Ktk Mioyo Yao,

Watu wengi kwa kuendelea kuacha su hii mioyoni mwao imewalete bp hata kuwaletea mauti ya kiroho na kimwili.

Ikumbukwe kutosamehe, ni moja ya mambo yanayoleta MUNGU kutokusikia hata maombi yako. maana imeandikwa usiposamehe Mungu hatakusamehe pia.

NAMNA YA KUSHINDA UCHUNGU

1-KUSAMEHE NA KUACHILIA.
Kusamehe ni kutangaza msamaha na kuachilia ni ile hali ya kutohesabu hatia tena aliyekukosea na hii huambatana na kusahau kabisa uliyotendewa na mtu huyo. math 6:14-15

2: KUOMBA MAOMBI YA TOBA.
>KUOMBA TOBA MWENYEWE.

Kumbuka matokeo ya kuchipuka au kuota kwa uchungu ni kupungukiwa neema sasa neema haipungui tu ila unakuwa umeshindwa kuishi ktk viwango vya utakatifu na MUNGU wako  kwa hiyo ni lazima uombe rehema ili urudi kwenye njia. yaani kile kiwango cha neema kiwe ktk hali yake ndipo uchungu utatoka ktk moyo wako. yakobo  1:5   "Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa hekima na aombe dua kwa Mungu"

3..KUBALI KUNYENYEKEA NA KUTII.

Matokeo ya kupungukiwa neema ni jibu la kukosa kunyenyekea.
biblia inasema  "  lakini MUNGU hutujalia neema iliyozidi;kwa hiyo husema,Mungu huwapinga wajikuzao bali huwapa neema wanyenyekevu"   yakobo 4:6.

kinachowafanya wengi kuishi kwa uchungu ni kule kukubali kunyenyekea na lulitii neno la MUNGU wengi hawataki kifuata hata ushauri watumishi wa MUNGU na neno .wamejihesabia haki hawataki kufuata maelezo hii imewaletea uharibifu wa haraka na kupotea kwa kichua maamuzi yasiyostahili..

Na ili uweze kwenda ktk njia njema na kuponywa na hili rudi ktk utii na neema itarudishwa mdani yako na hii ndio dawa hasa ya kupona kidonda hiki cha moyo wako.

Ni Vema Kutambua Hili  Na Mungu Akusaidie Kushinda Uchungu.

MUNGU AKUPE NGUVU YA KUVUKA KTK JAMBO HILI

MAWASILIANO.

NA MAOMBEZI.
0766891120

Jumamosi, 15 Agosti 2015

ELIMU/MAFUNDISHO YA MASHETANI.

Bwana YESU Asifiwe wana wa MUNGU leo imempendeza BWANA kujifunza somo hili linalohusu mafundisho ya mashetani.

NINI MAANA YA ELIMU/MAFUNDISHO YA MASHETANI?

Mafundisho ya mashetani ni mafundisho yanayofundishwa kinyume na mafundisho ya kweli ya kristo. Walimu wanaofundisha haya wanafundisha kinyume na injili ya kweli na huonesha wazi wazi kuwa kristo bado hajatutoa dhambini yaani hutufanya tujione bado sisi tuaminio hatujaamini au yanaonesha kazi ya msalaba kuea haijakamilika bado.  1timotheo  4:1-4 "  "

Biblia inasema  siku za mwisho watu watajitenga na imani ya kweli na kufuata mafundisho ya mashetani na biblia inaposema mafundisho ya mashetanihaimanishi kuwashetani au mashetani yanakuja yenyewe kufundisha bali yana watu wanaofanya kazi hiyo. Kumbuka watu  hujigeuza yaani wamejifanya kama watumishi watakatifu wa Mungu aliyehai..kumbuka watumishi wa ibilisi hujigeuza wafanane na watumishi wa kweli sio kwamba ndivyo walivyo bali wamejigeuza tu wawe mfano wa watumishi wa kweli ila sio halisia.

CHANZO CHA MAFUNDISHO YA MASHETANI
Mafundisho haya yanatokana na vyanzo hivi vifuatavyo.

1…Chanzo kwanza kabisa ni  ROHO ZIDANGANYAZO 1timoth 4:1
" Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati
za mwisho wengine watajitenga na imani,
wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya
mashetani
Roho hizi wakati mwingine huitwa roho mbaya na hii roho zina uvuvio wa pepo wachafu..kumbuka kuwa
"Roho ina uwezo wa kumsemesha mtu na kumwaminisha juu ya jambo fulani.Na kumfanya mtu aamini vilevile;
roho hizi ndizo hufanya kazi ya kutoa utabili wa uongo na huweza kuja kwa ndoto maono au kukusememesha kimya kimya.  yoh  8:43... .
8:43
" Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba
yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa
mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika
kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake.
Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe;
kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.
biblia inatueleza kuwa shetani ndiye mwanzilishi wa uongo na ndiye baba wa huo kwa hiyo utambue roho yake hufanya hayohayo, mhimu ujue hivi roho ya ibilisi hufanya uvuvio juu ya watu wake na huyatetanda mambo yao kwa nguvu ya huyo bila wao kujua..

NITAENDELEA

Jumatatu, 10 Agosti 2015

JE UNADHARAULIWA?

Watu wengi waliobeba Kusudi la Bwsna siku zote wamekuwa na changamoto ya kudharauliwa ktk yale wanayofanya;jambo hili limewavunja moyo wengi;limewatoa watu sana kwenye makusudi na kufanya washindwe kuendelea ma kile walichokuwa wamekusudiwa na Mungu

Nehemia    4:
1 Lakini ikawa, Sanbalati aliposikia ya kwamba
tulikuwa tukiujenga ukutuha, akaghadhibika, akaingiwa
na uchungu sana, akawadhihaki Wayahudi.
2 Akanena mbele ya nduguze na mbele ya jeshi la
Samaria, akisema, Wayahudi hawa wanyonge
wanafanyaje? Je! Watajifanyizia boma? Watatoa
dhabihu? Au watamaliza katika siku moja? Je!
Watayafufua mawe katika chungu hizi za kifusi,
nayo yameteketezwa kwa moto?
3 Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye,
akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda
mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe.

Shetani ana watu aliowaandaa kupinga au kuzuia kusudi pa Mungu hawa hupenda kuonesha kuwa wewe ni dhaifu sana na hauwezi ktk unalolifanya.

Unaweza kukutata na kikwazo hiki..adui yako kuona kazi yako ni dhaifu kuliko uhalisia wenyewe..rejea kauli ya tobia.

na wewe umekutana akina tobia wengi wao kazi yo ni kuvunja moyo na kuonesha kushindwa kuliko kushinda;wanapenda kukutiisha kwa vitisho na hata kukutungia mabaya..hakika hii ndiyo siri ya waovu kukuchimbia shimo ile ufe..

Lkn tambua hili wewe ambaye  alitenda kusudi ni wa maana sana;wewe umebeba dhamana na uhai wa jamii,taifa na familia yako ..wewe ndiye utaleta badiliko juu ya eneo hilo kiroho na kimwili ;usiogope wala kukuta tamaa shikilia tu neno la BWANA utafanikiwa;

Usiangangalie ziaka na dharau zao amini tu umebeba kitu cha thamani usikishushe njiani mpaka ufikishe mahali husika

Ni vigumu kujiamini wakati jamii,na watu na ulimwengu wanakuambia maneno na yanayoonesha dharau ya dhahiri kwenye maisha yako, lkn neno la Mungu linatuambia hivi USIOGOPE  isaya 43:1-4.
1 Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo,
yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope,
maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako,
wewe u wangu.
2 Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe;
na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika
moto, hutateketea; wala mwali wa moto
hautakuunguza.
3 Maana mimi ni Bwana, Mungu wako; Mtakatifu wa
Israeli, mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa
ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili
yako.
4 Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na
mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa
sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za
watu kwa ajili ya maisha yako.
5 Usiogope; maana mimi ni pamoja nawe; nitaleta
wazao wako toka mashariki, nitakukusanya toka
magharibi;
Dharau imeficha utukufu nyuma yake ,ukisoma neno hapo juu tugundua haya.

1®Wewe una kundi kubwa nyuma yako.
Bila kutambua hili watu wengi wanakata tamaa bila kujua kuwa kuna watu wengi wako nyuma yao kwani dharau ni jaribu linalokuja ili kukupima kama unaw eza kuongoza au la,kumbuka musa,alidharauliwa. YESU alidharauliwa na manabii wote walidharauliwa.

2®Wewe una vitu vya kipekee ..maana nyingine ni kwamba una vitu vya kipekee na tofauti na wengine.

Ukiangalia Mafarisayo walimwona YESU kama mtoto asiyehitaji heshima yao;wakamdharau kwa kuwa hakuwa na mambo kama yao bali alikuwa na hekima tofauti na hekima ya kifalisayo;ukiwa wa tofauti mwanzoni lazima udhalauliwe;utainekana mtu usiyefaa kwani wewe unalevel ambazo hazifanani na za kwao

wewe ujue hili Yesu aliyekuita anakutamvua usihangaike na mwanadamu songa mbele Bwana yuko pamoja nawe.